Ikiwa tayari ni Mzunguko wa 25, Tayari Wachezaji hawa wamefanikiwa kuoachika mabao 15 ,Huku zikibaki Mechi 5 tu msimu Huu kutamatika.
Wachezaji hawa Licha ya Kuwa ni viungo waushambuliaji, Wamekuwa na Wastani Mzuri wa Upachikaji wa Mabao , Huku Vita hiyo ikikolezwa na Nanafasi ya Msimamo wa Timu Zote mbili , Yanga aikwa nafasi ya Kwanza na Point 65, Huku Azam Akifatia na Alama 57.
Huenda Vita hii ikakosha Hisia za mashabiki na Wapenzi Wa Mpira, Na Endapo Mchezaji wa Azam Feisal Salum “Fei Toto” Atafanikiwa Kuchukua Kiatu Hicho , Itakuwa ni Mara Ya pili kwa Takribani misimu Mitano nyuma mfungaji bora wa Ligi kuu kutoka nje ya Timu ya Simba na yanga, Ikumbukwe Msimu wa 2021/2022 ,Kiatu hicho kilienda kwa Mchezaji George Mpole kutoka Geita Gold alie maliza Msimu na Magoli 16 ,goli moja Mbele Ya Mchezaji wa Young Africans Fiston Mayele.
Je Msimu 2023/2024 Ni nani ataibuka Mfungaji Bora wa Ligi kuu. Je Ni Aziz Ki au Feisal Salum.?
Muda Utaongea17:55