Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa Tsh. Milioni Mia moja kwaajili ya kuchangia Ujenzi wa Kanisa Jimbo kuu Katoliki Arusha, Parokia ya Mtakatifu Karoli Lwanga – Usa River wilayani Arumeru.
Akimuwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amewaambia waumini wa Kanisa hilo kuwa Rais Samia ametaka mchango wake huo Ukapatanishe, kuunganisha na kujenga Umoja wa Kitaifa.
Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa Mhe. Paul Makonda ametoa Mchango wa Tsh Milioni Kumi za Kitanzania na kuiombea sadaka yake hiyo iwe na baraka kwa wakazi wote wa Arusha kwa kutokuzaa Mapooza na kuitakasa Arusha dhidi ya Ajali za Barabarani ambazo zimekuwa zikiondoa Uhai wa watu wengi hususan watoto wadogo walio kwenye masomo.
Soma: Samia Aidhinisha Ajira Mpya 46,000
Mhe. Mkuu wa Mkoa ameombea pia Uzao wa Arusha kuwa wenye baraka na Neema,akihimiza wakazi wa Arusha kumtanguliza Mungu na kuwa na Hofu ya Mungu katika maisha yao ya kila siku ili kuendelea kuneemeka na baraka za Mungu.
Parokia ya Mtakatifu Karoli Lwanga ilianzishwa mwaka 1975 na kujengwa kanisa lililokuwa na uwezo wa kubeba waumini 600 kwa wakati mmoja na kulingana na wingi wa waumini kwasasa, Kanisa hilo limeamua kujenga kanisa jipya litakalokuwa na uwezo wa kubeba waumini 2500 kwa wakati mmoja.
Soma:Rais Samia Atoa Fedha Za Dharura Wizara Ya Ujenzi
Kulingana na Uongozi wa kanisa hili, Ujenzi wa jengo jipya ulianza mwaka 2010 ukiwa na makisio ya kutumia Shilingi Bilioni 2 na Milioni 700 mpaka kukamilika kwake.
Ikiwa ni muendelezo wa rais Samia Suluhu Hassan kutoa michango yake mbalimbali kwenye nyumba za ibada ili kuendelea kudumia imani na uchamungu.
Can you be more specific about the content of your article? After reading it, I still have some doubts. Hope you can help me.