Mamlaka ya Udhibiti Wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imearifu ongezeko la bei ya juu kwa bidhaa za mafuta ya petroli katika nchi kuanzia usiku wa leo Jumatano, Aprili 3, 2024, saa 6:01. Kwa mwezi wa Aprili 2024, bei ya rejareja ya mafuta katika Mkoa wa Dar es Salaam itakuwa shilingi 3257 kwa lita ya petroli, shilingi 3210 kwa dizeli, na shilingi 2840 kwa mafuta ya taa.
EWURA imeeleza kwamba ongezeko la bei kwa mwezi wa Aprili 2024 limetokana na kupanda kwa bei za mafuta ghafi (FOB) katika soko la kimataifa kwa asilimia 3.94 kwa petroli na asilimia 2.34 kwa dizeli, pamoja na kupungua kwa gharama za usafirishaji wa mafuta (premiums) kwa asilimia 4.28 kwa petroli na ongezeko la asilimia 0.76 kwa dizeli katika Bandari ya Dar es Salaam.
Vilevile, bei zimepanda kwa asilimia 13.73 kwa petroli na dizeli katika Bandari ya Tanga na asilimia 12.71 kwa mafuta yote mawili katika Bandari ya Mtwara.
“Kadhalika, ongezeko hili limechangiwa na kupanda kwa thamani ya kubadilisha fedha za kigeni kwa asilimia 3.19, ikichangiwa na kuongezeka kwa matumizi ya EURO kwa ajili ya malipo ya mafuta yaliyoagizwa,” EWURA iliongeza.
Read>>https://mediawireexpress.co.tz/dkt-biteko-ashuhudia-utiaji-saini-mikataba-uendeshaji-mradi-wa-eacop/
Read>>http://Dkt. Mwinyi Azindua Rasmi Uchimbaji Mafuta na Gesi Zanzibar
Aidha EWURA imewataka wafanyabiashara wa rejareja nchini kote kuuza bidhaa hiyo kutokana na bei elekezi iliyopo kwenye jedwali Namba 3 na wale wafanyabiashara wa jumla watumie jedwali namba 2 .
Hata hivyo Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji imewaonya wafanyabiashara wote watakao kiuka maelekezo kuwa haitosita kuwachukuliwa hatua kali za kisheria
Kwa kumbukumbu, bei za juu za bidhaa za mafuta ya petroli katika nchi hii ikiwa ni mara ya pili kufika kiwango kikubwa tangu mwezi tarehe 1 Nvemba 2023,kwa mwezi uliopita zilizoanza kutumika kuanzia Jumatano, Machi 6, 2024, saa 6:01, zilikuwa ni shilingi 3163 kwa lita ya petroli, shilingi 3126 kwa dizeli, na shilingi 2840 kwa mafuta ya taa katika Mkoa wa Dar es Salaam.
Thanks for sharing. I read many of your blog posts, cool, your blog is very good.