Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko leo tarehe 3 Aprili, 2024 amefanya mkutano na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Asasi ya Bodi ya Kimataifa ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia (EITI) ya nchini Norway, Mhe. Helen Clark. Katika mkutano huo uliofanyika kwenye Ofisi ndogo za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam.
Dkt. Biteko alieleza kuwa Tanzania inafanya juhudi za kuimarisha usimamizi wa rasilimali hizo muhimu ili kufikia viwango vya kimataifa na kudumisha ushirikiano kati ya EITI na Taasisi inayosimamia Rasilimali hizo nchini (TEITI).
Kwa upande wake, Mhe. Clark alisisitiza umuhimu wa ziara hiyo katika kuimarisha usimamizi wa rasilimali hizo nchini Tanzania ili kufikia viwango vya kimataifa vinavyohitajika kwa usimamizi bora wa rasilimali pamoja na kuendeleza ushirikiano kati ya EITI na TEITI.
Mbali na majadiliano ya serikali, Mhe. Helen Clark atakutana pia na wadau mbalimbali katika sekta hiyo nchini ili kujadiliana kuhusu changamoto na fursa za utekelezaji wa kanuni na taratibu za EITI, na kujadiliana kuhusu njia bora za kushirikiana katika kuhamasisha uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa rasilimali hizo.
Read>>http://President Samia woos Norwegian investors to Tanzania
Read>>http://President Samia begins official visit to Norway
Lengo la ziara hii ni kusaidia Tanzania kuimarisha usimamizi wake wa rasilimali za madini, mafuta, na gesi asilia, na pia kusaidia nchi kufikia viwango vya kimataifa katika usimamizi wa uwazi na uwajibikaji, huku ikiongoza kama mfano kwa mataifa mengine katika sekta hii.
Mhe. Helen Clark, ambaye amewahi kuwa Waziri Mkuu wa New Zealand na pia Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mipango ya Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), alihudhuria kikao hicho pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia Tanzania (TEITI) CPA.
Ludovick Utouh, Kaimu Katibu Mtendaji wa TEITI, Mariam Mgaya, Mkurugenzi Mkuu wa PURA, Mhandisi Charles Sangweni, pamoja na Mwakilishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Noel Kaganda.
Very nice post. I simply stumbled upon your weblog and wished to say that I’ve really loved surfing around your weblog posts. In any case I’ll be subscribing in your rss feed and I hope you write once more soon!
I don’t think the title of your article matches the content lol. Just kidding, mainly because I had some doubts after reading the article.