Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko, Leo 26 Machi, 2024, ameshuhudia Utiaji saini mikataba mitatu ya utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP).
Mkataba wa Kwanza unahusisha ukodishaji wa eneo la kujenga Miundombinu ya kuhifadhi mafuta (Land Lease Agreement for Marine storage and Terminal Area) Kati ya TPDC na EACOP.
Mradi wa pili ni wa kutumia eneo la Maji (Marine user Rights) kati ya EACOP na Mamlaka ya Bandari Tanga na mkataba wa tatu ni wa kufanya shughuli za Bandari (Marine Facility Agreement) Kati ya TPA na EACOP.
Utiaji saini mkataba huo pia umeshuhudiwa na Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda Mhe Dkt. Ruth Nankabirwa.