Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa amesema katika kipindi cha miaka mitatu Serikali imefanikiwa kukamilisha viwanja vya Ndege 5 ambavyo ni Kiwanja Cha Ndege cha Geita, Mwanza, Mtwara, Songwe na Songea.
Waziri Bashungwa ameeleza hayo jijini Dodoma tarehe 5 Aprili, 2024 katika hafla ya kuangazia mafanikio ya miaka mitatu ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Sekta ya Ujenzi.
Ameeleza miradi mingine ya Viwanja vya ndege vipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji ikiwemo Kiwanja Cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, Kiwanja cha Ndege cha Iringa, Kiwanja cha Ndege cha Kigoma (Awamu ya tatu), Kiwanja cha Ndege Moshi, Kiwanja cha Musoma, Kiwanja cha Ndege cha Sumbawanga, Kiwanja cha Ndege cha Shinyanga na Kiwanja cha Ndege cha Tabora (Awamu ya tatu).
Read>> http://President Approves 30 Billion for Emergency Road Repairs in the Country
Sambamaba na hilo Bashungwa amesema katika kipindi cha miaka mitatu wizara yake imefanikisha ujenzi wa madaraja makubwa 8 yakiwemo Daraja la Wami mkoani Pwani, Tanzanite,Gerezani Jijini Dar es Salaam, Daraja la Mpwapwa mkoani Dodoma, Daraja la Kiegeya mkoani Morogoro, Daraja la Ruhuhu mkoani Ruvuma, Daraja la Kitengule mkoani Kagera na Daraja la Msingi mkoani Singida.
Aidha, Madaraja matano yapo katika hatua mbalimbali za Utekelezaji ikiwemo Daraja la J.P Magufuli (Kigongo – Busisi) mkoani Mwanza ambao umefikia 85%, Daraja la Pangani mkoani Tanga umefikia 23%, Daraja la Mbambe mkoani Pwani umefikia 15% na Daraja la Mpiji Chini mkoani Dar es Salaam.
Read>> http://Ujenzi Wa Barabara Kilometa 60.7 Kiwango Cha Lami Misenyi – Bukoba
Thank you, I have recently been searching for info approximately this subject for a long time and yours is the best I have came upon till now. But, what in regards to the conclusion? Are you sure about the supply?
Merely wanna comment that you have a very nice web site, I like the style it really stands out.