Mtibwa Sugar ina historia kubwa kwenye soka la Tanzania ikiwa ni pamoja na kushinda ubingwa wa Ligi Kuu mara mbili katikati ya Simba na Yanga.
Hakuna asiekumbuka vipaji vilivyowahi kupita na kulelewa na baadae kuitumikia timu hiyo na hata kwenda kwenye timu kubwa kama Simba, Yanga na Azam kwaajiri ya kutafuta malisho mengine.
Zubery Katwila amekuwa Mchezaji na kocha wa timu hiyo , Beki Tegemeo wa Yanga Dickson Job, Kibwana Shomary Pamoja na kipa Abtwalib MShery ni mifano hai ya wachezaji ambao taifa inajivunia Mno kama mbegu zilizo zalishwa na kumwagiliwa hadi kukua kwake na sasa ni matumizi halali ya Timu ya taifa na hata vilabuni mwao.
Kwa bahati mbaya sana timu hio imekuwa katika mwenendo mbaya wa matokeo kwa misimu miwili mtawalia huku mpaka sasa ikiburuza mkia kwenye ligi na kuwa na viashiria vya kushuka Daraja
Uwepo wa Mtibwa Sugar Ligi Kuu umekuwa ni faida kubwa kwa vijana wa na wakazi wa mkoa wa Morogoro, vijana wengi wa Mrogoro wenye vipaji vya soka, Mtibwa imekuwa sehemu yao ya kutokea.
Kwa namna yoyote ile huwezi kuitenganisha Mtibwa Sugar na mpira wa mkoa wa Morogoro, Huwezi kutenganisha vipaji vya soka vya mkoa wa Morogoro na Mtibwa Sugar.Wakazi wa Morogoro wamenufaika kwa muda mrefu na uwepo wa Mtibwa Sugar kwenye Ligi Kuu, kuna faida nyingi zinazotokana na ujio wa timu nyingine kucheza Mtibwa, mashabiki pia kutoka mikoa tofauti wanaongeza mzunguko wa fedha.Kwa sasa Mtibwa Sugar ipo katika hali mbaya kwenye Ligi, kama ni mgonjwa basi anahitaji msaada wa haraka.
Mtibwa inaburuza mkia ikiwa nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa Ligi ikiwa na alama 17, Swali ni je Vipaji vya vijana wengi wa kitanzania vitaonekana tena wapi ilihali timu yenye desturi ya kukuza na kulea vipaji imeshuka daraja? , Swali hili tunawaachia benchi la ufundi na viongozi wa mtibwa katika juhudi binafsi kuibakisha timu hii ligi kuu Tanzania Bara
I dugg some of you post as I thought they were handy extremely helpful
Hello my loved one! I wish to say that this article is awesome, great written and come with approximately all significant infos. I?¦d like to look extra posts like this .