Wakati zikibaki Siku chache kufikia Siku ya Dabi ya Mzizima, (Simba Vs Azam), Wekundu wa Msimbazi Simba leo wameibuka Wababe Dhidi ya Mtibwa Katika mechi ya ligi kuu iliyowakutanisha Mapema leo saa 10 Alaasiri, Ambapo Simba Ameweza kuibuka na Ushindi wa Bao Mbili Kwa Bila Nakuzidi kuwasogelea Azam katika nafasi ya Pili.
Mabao hayo yamefungwa na Freddy Michael Koublan Dakika ya “35” na Saleh Karabaka dakika ya “64” Mabao yaliyowapatia Simba Ushindi na Kuweza Kufikisha Alama 50 Nyuma ya Yanga Walio na Alama 62, Na Azam Walio na Alama 64.
Soma Zaidi:Simba Sets Record For Worst Results
Ushindi Huu unaongeza Hisia kuelekea mechi ya Mei 9, 2024 Itayowakutanisha kikosi cha Azam Dhidi ya Kile cha Simba na endapo Azam atashinda mechi hiyo atazidi kuongeza Umbali wa Alama dhidi ya Simba na kuendele a kusalia katika nafasi ya tatu, Huku Simba akishinda Atazidi kuinusa harufu ya Nafasi ya pili katika ligi kuu ya NBCTanzania Bars.
Ikumbukwe katika Mzunguko wa Kwanza Timu hizi zilipo Kutana Matokeo yalikuwa ni sare ya Goli moja kwa Moja hali iliyofanya mzani kulingana. Je ni nani ataibukua Mshindi katika Michezo ujjao, Na nani atamaliza katika msimamo mzuri zaidi baina ya Timu mbili hizi za Dar es Saalam? Ni swala la muda tu.
Kikosi Cha Azam Kitashuka Dimbani badae Mida ya saa moja usiku kumenyana na Kikosi cha Timu ya Namungo katika Mchezo wa Robo fainali wa mashidnano ya Kombe la shirikisho la CRDB.
I am glad to be a visitant of this unadulterated web blog! , regards for this rare info ! .