Kocha wa Makipa wa Klabu ya Simba, Daniel Cadena ametoa shukrani kwa uongozi wa Simba ikiwa ndio mkono wa kwaheri ndani ya klabu hiyo, Cadena ameyasema haya kupitia ukurasa wake wa instagram.
“Asanteni nimeifahamu SIMBA na nimehisi mapenzi yangu kwa klabu hii kubwa Siwezi kusema chochote kibaya juu ya klabu hii, imenisaidia kila wakati hata katika nyakati mbaya”
View this post on Instagram
“Najua haikuwa rahisi kukufanyia uamuzi huu, lakini sasa ni wakati wa kuunganisha nguvu na kuisafisha Simba kwa pamoja kwa manufaa ya siku zijazo za Simba”.
Kila la kheri kwa familia ya Simba, – Cadena
Soma: Simba Kamiligado, Yaenda Kujifua Zanzibar
Sambamba na hilo Daniel Cadena amempongeza Mohamed Dewji (MO) Kwa ujasiri wake wa kutoa maamuzi magumu ya kuijenga timu ya Simba.
Mimi na wewe @moodewji tumezungumza mara moja tu, na umenionyesha kuwa mnyenyekevu na wakati huo huo jasiri kufanya maamuzi katika nyakati ngumu. 👌
Kwa miradi imara na misingi imara inakupasa kufanya maamuzi magumu bila kutumia moyo wako. 💪
Kwa wafanyikazi wote:
“Ikiwa unastahili, uko Simba, ikiwa haufai, uko mitaani.”
View this post on Instagram
Ninakuamini na njia yako ya kusimamia. Nakutakia kila la kheri kwako na kwa Simba ambayo nayo ni bora kwa familia ya SIMBA. Cadena
49 Comments