Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa amefanikiwa kumaliza mgogoro wa wakazi wawili ambao ni Victoria Chiwangu na Hillary Temu wa jijini Arusha ambao hapo awali Hillary alijenga kwenye kiwanja cha Victoria namba 313 Kitalu F Njiro, Arusha.
Hillary alipewa muda wa kukaa chini na Victoria ili wakubaliane kabla ya kuchukuliwa hatua za kuvunjiwa nyumba aliyojenga kwa mwenzake iwapo angekaidi.
Hata hivyo Hillary alikubali kumlipa Victoria kwa awamu na tayari ameisha mlipa sehemu ya fedha.
Waziri Silaa amemaliza mgogoro huo kwa kuwakutanisha wakazi hao katika Kliniki ya Ardhi iliyofanyika jijini Arusha ambapo hapo awali Waziri Silaa aliahidi kwenda kusimamia uvunjaji wa nyumba ya Hillary Temu.
Wakazi hao walikuwa na miaka 13 hawajasalimiana wala kushikana mikono, jambo ambalo Waziri Silaa alilimaliza kwa kuwapatanisha ndani ya dakika chache.