Wakili na mwanaharakati wa haki za binadamu, Maduhu William, amekemea ukatili dhidi ya watu wenye u albino na kutaka jeshi la polisi likomeshe matukio hayo.
Amesema hayo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio la kutekwa mtoto mwenye ualbino mkoani Kagera.
Soma Zaidi:Vijana Watakiwa Kuchangamkia Fursa Mbadala
“Ninaalani tukio hilo na pia ninatoa wito kwa jeshi la polisi kuharakisha uchunguzi na kuwakamata wahusika.
“Amesema, 31 mwaka huu, mtoto mwenye ualbino wa miaka kama miwili na nusu alichukuliwa kwa nguvu kutoka mikononi mwa mama yake na watu wasiojulikana, lakini hadi sasa hajapatikana.
Amesema, tangu wakati huo haijulikani kama mtoto huyo yuko hai au ameuawa, na kwamba ni muhimu vyombo vya dola kufanya kazi haraka ili wahusika wapatikane na mtoto ajulikane alipo.
“Inauma sana kuona Watanzania bado tunaendekeza mila zisizo na maana. Jeshi la polisi liharakishe uchunguzi tujue waliohusika wakamatwe,” amesema
Amefafanua kuwa pamoja na kwamba baba wa mtoto huyo tayari amekamatwa, anaamini kwamba msako zaidi unahitajika.
“Lakini pia wabunge nao walipe nguvu tukio hili, ikiwezekana wasimamishe shughuli za bunge walijadili kwa kina,” amesema.
Amesema, wabunge wakilijadili tukio hilo kwa kina litakuwa na msukumo mkubwa na hatimaye matukio ya kuteka albino ba kuwaua yanaweza kuisha.
“Pamoja na hayo, nitoe wito wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mkuu wa Jeshi la Polisi kwamba zikipita siku saba kuanzia sasa bila kujulikana hatma ya mtoto huyo, basi ni vyema waachie ngazi,” amesema.
William alifafanua kuwa hatua hiyo inamhusu pia kamanda wa polisi wa mkoa ambao tukio hilo