Rais Samia Suluhu Hassan amezindua Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi pamoja na Mifumo ya Usajili na Malalamiko ya Ukiukwaji wa Misingi ya Ulinzi wa taarifa binafsi leo April 03,2024 Jijini Dar es salaam na kusisitiza kuwa kila Binadamu ana utashi na ana stahili staha hivyo zipo baadhi ya taarifa ambazo angependa zisijulikane kwa kila Mtu ndio maana imeanzishwa sheria na Tume ya kulinda faragha za Watu.
Rais Samia amenukuliwa akisema “Miaka ya nyuma ingawa sio nyuma sana huko Duniani kuna visa vilitokea vinavyohusisha kuvuja kwa taarifa binafsi, mifano ya taarifa zinazochukuliwa na Hoteli au Hospitali kuhusu Wateja kuvuja na kuleta athari kwa Wahusika, kuna mifumo ya Kampuni binafsi kutafuta taarifa binafsi za Watu kinyume cha haki za Watu il watumie taarifa hizo kwa maslahi yao ya kibiashara, pia kuna mifano kuhusu vitendo vibaya vilivyowahi kufanywa na Watu kudukua mifumo na kukusanya taarifa binafsi, pindi haya yakibainika yanaonesha ukiukwaji wa haki za Watu”
Read>>http://Tanzania close to adopting new broadcasting technology
Read>>http://Nape Appoints New TCRA Board Members
“Haya yote yalisababishwa na udhibiti hafifu wa mifumo ya ukusanyaji, utunzaji na utumiaji wa taarifa binafsi katika Taasisi mbalimbali zilizokusanya na kutumia taarifa binafsi, katika kukabiliana na haya yote ndio maana tupo hapa leo kuzindua Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ambapo Katiba ya Tanzania imeweka bayana kulindwa kwa haki za Binadamu ikiwemo kulindwa haki ya faragha, kupitia Ilani ya CCM, Chama kiliahidi kuongeza ulinzi wa faragha na taarifa za Wananchi kwa kukamilisha kutunga sheria ya kuimarisha ulinzi na taarifa na takwimu ambapo ahadi hii tulitimiza mwaka 2022”
“Kila Mwanadamu ana utashi na ana stahili staha hivyo zipo baadhi ya taarifa ambazo angependa zisijulikane kwa kila Mtu na kwakweli ingekuwa taarifa zetu zote zipo wazi na Watu wanazijua tusingetazamana usoni au hii Dunia ingekuwa Dunia ya aina nyingine, ndio maana tumekuja na sheria hii ili kutunza utu wa Mwanadamu”
“Zipo taarifa binafsi zinaweza kusababisha unyanyapaa kwa mfano Daktari aliyekosa uadilifu akitoa taarifa za ugonjwa wa Mtu iwe wa kurithi au ugonjwa fulani unaweza kuleta unyanyapaa, pia unaweza kutoa taarifa ya Mtu ikaleta vita na vurugu, kuna umuhimu wa kuanzisha sheria na Tume hii”