Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amefunguka kwa hisia alipo ulizwa na waandishi wa habari kuhusu kuondoka kwa mpinzani wake wa muda mrefu EPL Jurgen Klopp [Kocha wa Liverpool]
Pep amekiri hayo jana baada ya kumalizika kwa mechi kati ya Man City na West Ham United huku timu hiyo ikiibuka na ushindi wa goli tatu kwa moja na kutawazwa rasmi kuwa mabingwa wapya wa EPL huku wakichukua ubingwa huo mara nne mfululizo,
Soma Zidi:EPL Kumalizika Leo kwa Michezo 10
katika mahojiano hayo Guardiola alisema kuwa Klopp amekuwa na mchango mkubwa katika kazi yake ya ukocha na atamkumbuka daima na ataendelea kumheshimu kama moja ya makocha wenye mafanikio makubwa sana katika ligi hiyo yenye ushindani na mvuto zaidi dunani
Pep ameongeza yakuwa anahisia kuwa Klopp atarudi tena katika ligi hiyo ya uingereza
“Ninahisia kubwa kuwa Klopp atarudi tena EPL” alisema Guardiola
Ikumbukwe ni wiki chache zimepita baada ya kocha huyo kutangaza kuondoka katika timu ya Liverpool baada ya kukaa kwa na kuiongoza timu hiyo kwenye mafanikio mengi kama meneja wa timu hiyo
Tazama Zaidi:Pep Azungumza kwa hisia kuuondoka kwa Klopp EPL”Nitamiss Sana”
na mara kadhaa moto umekuwa ukiwaka pale timu hizi mbili [ManCity na Liverpool] wakikutana huku makocha hao wakivimbishiana vifua kwa kuonesha ubora wa mbinu kadha wa kadha wakiwa uanjani
Man City Wamehitimisha msimu wakiwa na Alama 91 huku Liverpool akiwa katika nafasi ya tatu na alama 82 nyuma ya Arsenal 89.
Jurgen Klopp anaondoka Liverpool akiwa na heshima ya kuwapatia majogoo wa London takribani makombe 8 ya ligi kuu na amekuwa mshindani mkubwa wa Guardiola aliyevunja rekodi jana ya kuwa kocha wakwanza katika ligi hiyo kuchukua mara nne mfululizo makombe ya ligi kuu ya uingereza mfululizo.