Ligi kuu ya NBC Tanzania bara itampokea mgeni aliyepotea kwa muda mrefu kwa miakaka takribani 22 , tangu mwaka 2002 ambapo ni mara ya mwisho timu hiyo kushiriki ligi kuu.
Pamba ya Mwanza imerejea Ligi Kuu baada ya kuifunga Mbuni ya Arusha bao 3-1 huko Jijini Arusha na kufikisha alama 67 ambazo zaidi ya Ken Gold ambayo imeshapanda daraja hakuna nyingine inaweza kufika hapo.
Soma Zaidi;Bilioni 19.7 Kukarabati Uwanja Wa Uhuru
Pamba iliyowahi kuwa moja ya timu vigogo hapa Tanzania ilishuka daraja miaka mingi na kushindwa kurudi Ligi Kuu pamoja na jitihada mbalimbali zilizo fanywa na uongozi wa timu hiyo tangu miaka hiyo hadi sasa
Moja ya changamoto iliyokuwa kikwazo kikubwa cha timu hiyo kutopanda daraja kwa muda mrefu ni pamoja na ukata wa pesa za kuiendesha timu, hususa ni katika uwekezaji wa mpira wa kisasa.
Timu nyingi zipandazo daraja zimekuwa zikikumbana na changamoto ya kupambana na kasi ya mabadiliko yaliyopo katika ligi kuu, hasa kwenye upande wa uwekezaji wa benchi la ufundi na hata wachezaji na kufanya timu hizo kushika mkia katika ligi na hata kuporomoka tena na kurudi katika Championship.
Media Wire imewauliza wadau kadhaa wa michezo kutaka kujua Wanaiona wapi timu hii ya pamba na Kuishauri nini ili iendelee kubaki misimu ijayo baada ya kumalzika kwa Msimu ujao wa ligi kuu?
Jackson Samson ,Mdau wa michezo ameishauri timu hiyo kuhakikisha inaweka mkazo kwenye usajili wa benchi la ufundi na wachezaji kwa lengo la kuhakikisha inapata makocha na wachezaji wazoefu na wenye uwezo wa kupambana na kuiweka katika sehemu nzuri ya msimamo msimu ujao.
“Unajua uwekezaji ndio kila kitu, siisemi vibaya timu ya mashujaa kutoka Kigoma, Lakini ninashaka na Usajili pamoja na uwekezaji wake, Angalia nafasi iliyopo na ni punde tu baada ya kupanda daraja msimu uliopita, Haya Yawe funzo kwa Pamba, watafute wawekezaji wapambane ili timu ikipanda ipeperushe vyema bendera ya Jiji la Mwanza” alisema Jackson Samson.
Pili Imelda, Mdau wa Mpira kutoka Mbezi Juu Dar es salaam, Ameipongeza klabu hiyo na kuishauri isisajili tu wachezaji bora bali isajili wachezaji wenye ubora na moyo wa kuipambania timu hiyo.
“Unaona kuna timu fulani ya Kariakoo, Si kwamba haina wachezaji bora , la hasha ila inawachezji walio na morali ya chini mno, hii inainyon’yesha timu, kwahio Pmba ikipata wachezaji kama hao ni haraka mno kushuka daraja tena, kwahio wawe makini mno katika hilo”
Hongera sana wachezaji, viongozi, mashabiki na wanachama wa timu ya Pamba bila kusahau chama cha soka cha Jiji la Mwanza MRFA kikiwa chini ya Hepafra Lufano kama Mwenyekiti.
Your article helped me a lot, is there any more related content? Thanks!
Hello There. I found your blog using msn. This is a very well written article. I’ll be sure to bookmark it and come back to read more of your useful info. Thanks for the post. I will certainly comeback.