Waziri wa Ardhi, Jerry Slaa, amefanikiwa kufanikisha operesheni ya kuwatia mbaroni watuhumiwa watatu wanaodaiwa kuwa matapeli sugu wa ardhi katika Wilaya ya Temeke. Matapeli hawa wamekuwa wakiendesha biashara haramu ya kuuza maeneo ambayo ni mali ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), na kujipatia faida kubwa kwa njia ya udanganyifu.
TAZAMA:
Kufuatia mkakati wa mtego ulioandaliwa kwa ushirikiano wa karibu kati ya Wizara ya Ardhi na NSSF, watuhumiwa hao walikamatwa wakati walipokuwa wakijaribu kufanya mauzo ya ardhi kwa bei ya juu ya Shilingi Milioni nane.
Waziri Slaa ametoa wito kwa wananchi kuepuka kununua ardhi chini ya usimamizi wa viongozi wa serikali za mitaa, na amewataka wenyeviti wa serikali za mitaa kusitisha mara moja biashara haramu ya kuuza ardhi.
Meneja Miliki wa NSSF, Geoffrey Timoth, alithibitisha kupokea taarifa za matapeli wanaohujumu maeneo ya mfuko kwa njia mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuyauza au kuvamia kinyume cha sheria. NSSF sasa imeanzisha zoezi la kubomoa nyumba zilizojengwa kinyume cha sheria.Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Malela, Kata ya Tuangoma, Wilaya ya Temeke, Owing Henry Mkinga, alilaani vitendo vya utapeli vinavyofanywa na baadhi ya viongozi wasio waaminifu katika serikali ya mtaa. Amesema kuwa matapeli hao wamekuwa wakishirikiana na baadhi ya wajumbe wa serikali ya mtaa.
Hii ni hatua muhimu katika jitihada za Waziri Slaa katika kutatua migogoro ya ardhi nchini, na ni wito kwa wananchi wote kushirikiana na serikali katika kuzuia vitendo vya udanganyifu katika masuala ya ardhi.13:01