Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amesema hadi kufikia March, 2024 jumla ya ratiba za mabasi 798 zimetolewa kwa ajili ya safari za usiku akisema hiyo ni ishara kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeonesha dhamira ya kweli ya kuifungua Nchi kiuchumi.
Soma Zaidi:Tragic Accident Claims 15 Lives in Arusha
Akiwasilisha Bungeni Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 leo May 06,2024, Mbarawa amesema “Utakumbuka kuwa, tarehe 28 Juni 2023, Mh. Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alitangaza hapa Bungeni uamuzi wa Serikali wa kuondoa zuio la mabasi
ya abiria kusafiri nyakati za usiku lililowekwa mwaka 1994”
“Napenda kulitaarifu Bunge lako tukufu kuwa Serikali kupitia Wizara ya Uchukuzi na LATRA ilifanya maandalizi na kuanza kutoa ratiba za mabasi kusafiri nyakati za usiku kuanzia tarehe 1 Oktoba, 2023”