Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa, ameonya matumizi mabaya ya magari ya serikali ikiwa ni pamoja na kubeba mkaa na maharusi.
Akikabidhi magari 16 yenye thamani ya zaidi ya Sh 2 bilioni yaliyotolewa kwa ajili ya kuimarisha Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP), Silaa ametaka magari hayo yatumike kwa kazi ya mradi na si vinginevyo.
“Magari haya yatumike kwa kazi ya mradi, wale wote watakaokabidhiwa magari haya wayatumie vizuri, wayatunze, napenda kuyaona yanafanya kazi na kuongeza kasi ya utekelezaji wa uboreshaji wa milki, kazi ya matumizi bora ya ardhi Vijijini na kazi ya urasimishaji katika Halmashauri Mijini”
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Anthony Sanga amesema mradi huo unaotekelezwa Nchini chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi unagharimu zaidi Sh 346 bilioni ambazo ni sawa na dola za Marekani milioni 150.
Mratibu wa Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) Joseph Shewiyo amesema mradi huo unajukumu la kusimamia usalama wa milki za ardhi mijini na Vijijini ambapo amewahamasisha Wanandoa wawe na umiliki wa ardhi wa pamoja akisema mradi huo unatekelezwa katika Halmashauri 36, mitaa 660, Vijiji 1700 na umetoa ajira kwa Watumishi 700 ambao wanafanyakazi katika Halmashauri hizo.
Very fantastic visual appeal on this website , I’d value it 10 10.