Dark
Light

Bilioni 19.7 Kukarabati Uwanja Wa Uhuru

Akizungumza na Wadau na Viongozi Mbali Mbali wa sekta ya Michezo Waliohudhuria katika utiaji saini wa ukarabati huo Leo April 25/04/2023 kati ya Serikali na Kampuni ya Ukandarasi ya CRCEG ,Katibu Mkuu wa wizara ya Utamaduni, Sanaa Na Michezo Ndug, Gerson Msigwa Amesema Uhitaji wa Viwanja Ni Mkubwa Na Seeikali Imeongea na Kampuni Hiyo Kuhakikisha Anamaliza Ndani ya Miezi sita Badala ya Marekebisho Hayo Kukadiriwa Kuisha Baada ya Miezi 12.
April 25, 2024
by

Neema Imeendelea kumwagika katika sekta ya michezo ikiwemo ukarabati wa viwanja Mbali Mbali na sasa Uwanja wa Uhuru uliopo Pembezoni kidogo mwa uwanja wa Mkapa Utafanyiwa marekebisho makubwa Huku shilingi Bilioni 19.07 Zikielekeza kutekeleza Adhma ya ukarabati Huo.

Akizungumza na Wadau na Viongozi Mbali Mbali wa sekta ya Michezo Waliohudhuria katika utiaji saini wa ukarabati huo Leo April 25/04/2023 kati ya Serikali na Kampuni ya Ukandarasi ya CRCEG ,Katibu Mkuu wa wizara ya Utamaduni, Sanaa Na Michezo Ndug, Gerson Msigwa Amesema Uhitaji wa Viwanja Ni Mkubwa Na Seeikali Imeongea na Kampuni Hiyo Kuhakikisha Anamaliza Ndani ya Miezi sita Badala ya Marekebisho Hayo Kukadiriwa Kuisha Baada ya Miezi 12.

Read More:Tanzania to Build State-of-the-Art AFCON Stadium in Arusha

“Tumekuwa makini Mno katika Uchaguzi wa Mkandarasi na Kampuni hii(CRCEG) , imekuwa Hapa kwa muda na Tunaimani Itafanya kazi Nzuri” Amesema Msigwa.

Pia ameongeza kuwa marekebisho hayo yamelenga Kuongeza Viwanja Vyenye Ubora wa CAF Tanzania : Ikiwa ni Maandalizi ya Michuano ya AFCON 2027 Ambapo Tanzania Itakuwa mwenyenji ikishirikiana na Kenya pamoja na Uganda.

Msigwa Amedokeza Maendeleo ya ukarabati Wa uwanja wa Mkapa kuwa yapo Katika hatua ya Asilimia 25, na Wakandarasi wanafanya Kazi kukimbizana na Muda ili Viwanja hivyo Vianze kutumika Mapema.

Pia Msigwa Amesema Serikali Chini ya Rais Samia ipo katika Mpango wa Ujengwaji wa Vituo vya Michezo Nchi nzima ili kutanua Fursa ya kupata vijana wengi katika sekta Ya Michezo.
” Serikali inataka kila mtu mwenye Uwezo wa Mpira aoneshe kipaji chake Tukione kupitia Vituo hivyo” Amesema Msigwa.

Pia Rais Wa Shirikisho La Mpira Tanzania (TFF) Ndg. Wallace Karia Ameishukuru Serikali Kwa Ukarabati huo Kwani Utakuza Michezo Tanzania Hasa katika Nyanja ya Miundo Mbinu.

“Uhuru ni Uwanja wa Kihistoria , Hapa ndipo bendera ya Mwingereza  ilishusha na bendera ya Tanganyika ilipandishwa ,Tunaishukuru Serikali kwa Kufikia maadhimio ya Kuuboresha ” Aliongeza Wallace Karia

“Uwanja huu hautatumika tu kwenye mpira wa miguu, bali hata michezo mingine kama masumbwi pamoja na riadha”

3 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Don't Miss

Ibrahim Traoré Captivates Audience At Mahama’s Inauguration

Captain Ibrahim Traoré, the interim president of Burkina Faso,  will

Tanzania Awaits Arrival of New Buses for BRT

Tanzania is eagerly anticipating the arrival of 250 new buses