Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amekutana na mwanamuziki maarufu wa Korea Kusini, Bw. Cho Yong-pil, ikiwa ni sehemu ya ziara yake nchini Korea Kusini. Mkutano huu unalenga kuimarisha mikakati ya kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania kwa kutumia nyanja mbalimbali, ikiwemo muziki.
Bw. Cho Yong-pil, ambaye ni mmoja wa wanamuziki wenye ushawishi mkubwa nchini Korea Kusini, amekuwa kwenye tasnia ya muziki kwa zaidi ya miaka 50. Akiwa na sifa kemkem, ameshinda tuzo nyingi kupitia kampuni yake ya YPC na kupata umaarufu mkubwa ndani na nje ya Korea Kusini. Muziki wake umevuka mipaka na kuvutia mashabiki wengi ulimwenguni kote.
Katika mazungumzo yao yaliyofanyika Seoul, Bw. Cho alimweleza Rais Samia jinsi anavyoipenda Tanzania na alivyojawa na shauku ya kurejea tena nchini humo kabla hajaondoka duniani. Alisema kuwa Tanzania ina nafasi maalum moyoni mwake, hali iliyopelekea kuimba nyimbo mbili maarufu kuhusu nchi hiyo, “Leopard of Kilimanjaro” na “Like Serengeti.” Nyimbo hizi zimekuwa maarufu si tu Korea Kusini, bali pia katika sehemu mbalimbali duniani, na zimechangia pakubwa kuitangaza Tanzania kama kivutio cha kipekee cha utalii.
Soma Zaidi: Rais Samia Awakutanisha Wataarishaji na Waigizaji Filamu Korea & Tanzania
Rais Samia alimshukuru Bw. Cho kwa jitihada zake za kuitangaza Tanzania kupitia muziki wake. Alisema kuwa nyimbo hizo zimekuwa na athari kubwa katika kukuza na kueneza taarifa za vivutio vya utalii vya Tanzania, hususan Mlima Kilimanjaro na Hifadhi ya Serengeti. “Nyimbo zako zimebeba uzuri wa nchi yetu na kuusambaza kwa ulimwengu, tunakushukuru sana kwa mchango wako,” alisema Rais Samia.
Aidha, Rais Samia alimsihi Bw. Cho arejee Tanzania ili atunge nyimbo nyingine zaidi kuhusu vivutio mbalimbali vya utalii na utamaduni wa Tanzania. Alisema kuwa Tanzania ina vivutio vingi vya kipekee vinavyostahili kutangazwa kimataifa ili kuvutia watalii zaidi na kuongeza mapato ya nchi kupitia sekta ya utalii. Vivutio hivi ni pamoja na Zanzibar yenye fukwe za kuvutia, Hifadhi ya Ngorongoro, na maeneo mengine mengi yenye mandhari nzuri na utajiri wa utamaduni.
Bw. Cho aliahidi kuzingatia ombi hilo na kuongeza kuwa Tanzania ni nchi yenye utajiri mkubwa wa maliasili na utamaduni ambao unastahili kuimbwa na kutangazwa zaidi. Alisema kuwa anaamini muziki unaweza kuwa chombo muhimu cha kuunganisha watu na kuvutia watalii kutembelea Tanzania na kushuhudia uzuri wake wenyewe.
Ziara ya Rais Samia nchini Korea Kusini imeonekana kuwa na umuhimu mkubwa katika juhudi za Rais za kutangaza utalii wa Tanzania kimataifa. Serikali ya Tanzania imekuwa ikitafuta njia mbalimbali za kuboresha na kutangaza sekta ya utalii, ikiwemo kutumia wasanii maarufu na watu wenye ushawishi katika jamii za kimataifa. Kwa kupitia mikakati kama hii, Tanzania inaendelea kujipambanua kama moja ya nchi za Kiafrika zenye vivutio vya kipekee na zinazostahili kutembelewa na watalii kutoka pande zote za dunia.
I do not even know how I ended up here, but I thought this post was great. I do not know who you are but definitely you are going to a famous blogger if you aren’t already 😉 Cheers!
Hello there, You’ve done a great job. I’ll definitely digg it and personally suggest to my friends. I am sure they’ll be benefited from this site.