Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekutana na viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini, ofisini kwake Mlimwa jijini Dodoma, katika jitihada za kutatua changamoto za kodi zinazowakabili wafanyabiashara.
Kikao hicho kimefanyika siku ya tatu tangu wafanyabiashara hao walipofunga maduka yao, wakilalamikia mzigo mkubwa wa kodi ambao wanasema unawakosesha uwezo wa kufanya biashara kwa faida. Wafanyabiashara wamekuwa wakidai kuwa kodi za TRA zimekuwa kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya biashara zao, na wameomba serikali kusikiliza kilio chao na kuchukua hatua za kupunguza mzigo huo.
Waziri Mkuu Majaliwa, akizungumza baada ya kikao hicho, ameahidi kuwa serikali itashirikiana na sekta binafsi kutafuta suluhisho la kudumu kuhusu kodi. Amesema serikali inatambua changamoto za wafanyabiashara na itafanya kila linalowezekana kuhakikisha mazingira bora ya biashara yanapatikana.
SomaZaidi;Mapambano Dhidi ya Wanyamapori Wakali
Hata hivyo, suala la kodi limeendelea kuwa tatizo kubwa kwa wafanyabiashara nchini Tanzania. Wafanyabiashara wanaamini kupunguza mzigo wa kodi kutawawezesha kuongeza uzalishaji na kuboresha huduma zao kwa wateja.
Serikali imeahidi kuendelea kushirikiana na wafanyabiashara ili kujenga mazingira mazuri ya biashara ambayo yanazingatia maslahi ya pande zote na kuhakikisha ushirikiano endelevu katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini.
Kikao cha leo kati ya Waziri Mkuu Majaliwa na viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara kimeweka msingi wa majadiliano ya kina kuhusu namna bora ya kushughulikia kero za kodi na masuala mengine yanayohusu biashara nchini Tanzania. Wafanyabiashara wanasubiri kwa hamu hatua zaidi za serikali kutekeleza ahadi zilizotolewa na kuhakikisha mazingira bora ya biashara yanapatikana haraka iwezekanavyo.
Very nice info and right to the point. I don’t know if this is actually the best place to ask but do you folks have any thoughts on where to hire some professional writers? Thank you 🙂