Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi, Amekoshwa na Bunifu Mbali mbali Za wanachuo Wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Alipo shiriki kama Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Kongamano la Maadhimisho ya Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere, lililofanyika Jumatatu Aprili 8, 2024 katika Ukumbi wa Utamaduni wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Kigamboni, Dar Es Salaam, ambalo lilijumuisha watu mbalimbali, ambapo kabla ya hapo, alitembelea mabanda na kujionea maonesho ya ubunifu katika masuala mbalimbali unaofanywa na wanafunzi wa chuo hicho.
More On:
Lengo la Maadhimisho Haya Ni Kuenzi, Kuishi, kuhifadhi na kuendeleza mafundisho, falsafa, na maono kwa Kuwafundisha vijana juu ya maono na falsafa aliyokuwa nayo Mwalimu Nyerere kuhusu uongozi bora, maendeleo ya taifa, na umoja wa kitaifa Utakao Saidia Ustawi wa Taifa katika Nyanja Za Kiuchumi, Kisiasa na Hata Kiutamaduni.
Akihutubia katika kikao hicho Dkt. Nchimbi Amezifu Falsafa, uaminifu na Kujitoa kwake kwaajiri ya Nchi Jambo lililopelekea kumfanya Kuwa Kiongozi Bora Wa Tifa Lake
“Nataka niwaambie Kwa Dhati Kabisa Nchi hii Imewahi Kupata kiongozi bora basi, Baba wa Taifa ni namba moja, Na Mimi Sioni Haya Hata Kidogo Kwasababu Mimi ni mfuasi wa Mwalimu kwasababu Mapenzi yake katika Nchi yake,uaminifu na kujitoa kwake juu ya Nchi yake havikuwa na shaka hata kidogo, Kama kunamtu alikuwa anakubalika katika Nchi basi ni mwalimu Nyerere” Dkt, Nchimbi
DK.Nchimbi Ameongeza Kuwa Bunifu Za Wanachuo Hao Zitasaidia Katika Kuleta Na Kukuza Uchumi Wa Taifa la Tanzania Na Kiyatimiza Maono Ya Hayati Julius Nyerere Katika Kuvumbua, Kukuza Na kulinda Vumbuzi Na Ubunifu Wa Watanzania Kwa Maendeleo ya Taifa Zima.
Maadhimisho Haya Yameongozwa na Mada Mbali Mbali zilizolenga Kumuenzi Baba Wa Taifa Aliyezaliwa Takribani Miaka 102 iliypita Mnamo April 13 1922 na Kila Mwaka Taifa linaendelea kuyaenzi mema aliyoyafanya kama Rais Wa kwanza Wa Nchi ya Tanzania, na Taifa Hufanya Kumbukizi ya Kifo chake kila Mwaka Tangu alipo fariki October 1999.
Source: Chama Cha Mapinduzi.
Post Views: 28