Meneja wa habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba ,Ahmed Ally ameandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa Instagram kuhusu wakati mgumu wanaokutana nao klabu hiyo kutokana na kuongezwa chumvi kwa watu.
Ahmed Ally ameandika maneno hayo baada ya kutolewa na timu ya Mashujaa katika mashindano ya CRDB Confederation Cup ikiwa ni muendelezo wa matokeo mabaya baada ya kutolewa Ligi Ya Mabingwa Afrika hatua ya robo fainali
“Timu yetu inapitia kipindi kigumu Lakini ni tofauti na inavyozungumzwa yaani wanaongeza chumvi
Huu ni mpango wa makusudi unaoratibiwa na wasiotutakia mema, Bahati mbaya ni kwamba Wana Simba tumeingia kwenye mtego wa kujidharau na kujitukana
Tukiwa na Simba Bora sana tuliwahi kutolewa hatua ya awali ya ligi ya Mabingwa Afrika na UD Songo, Tukiwa na Simba Bora tuliwahi kutolewa na Green Warrios kwenye Kombe la Shirikisho
Haya mi Maisha ya kawaida kwenye mpira wa miguu
Kila timu ya mpira hupitia nyakati kama hizi, Ila tukipitia Simba basi huonekana ni kitu cha ajabu inawezekana tunahukumiwa na ukubwa wetu
Read>> Simba all set for showdown with Mashujaa in Kigoma today
https://mediawireexpress.co.tz/simba-all-set-for-showdown-with-mashujaa-in-kigoma-today/
Leo watakuambia wachezaji wabovu, kesho Muwekezaji tatizo, kesho kutwa Viongozi hawafai
Hivi tungekua na matatizo yote hayo si tungekua tumeshuka daraja?
Wengine wanaibuka kukashifu viongozi na kudhihaki wachezaji wakiamini huko ndio kuipenda Simba au wao ndio wenye uchungu sana na Simba
Wakati Nyuma Mwiko wako dhofli hali waliibuka na kauli ya kusema tumeipenda wenyewe acha ituue, Hii ilikua kauli ya kishujaa sana na waliamua kufa na timu yao
Read>> Embrace constructive criticism – Mangungu tells Simba
https://mediawireexpress.co.tz/?s=simba
Kwa sasa hatuna budi kusimama na timu yetu ili mambo yasiharibike zaidi, hatuwezi kubadili yaliyopita ila tunaweza kutengeneza yajayo
Tulichobakiwa nacho ni Ligi Kuu ya NBC, Kwa pamoja tuwekeze nguvu kwenye kombe hili
Tuache kulaumiana, tuhamishie machungu yetu na tuelekeze hasira zetu kwenye ligi
Pengo ni alama 4 tukisimama sawa sawa kwa umoja wetu tunaliondoa
Hii inaanza na mechi ya Tarehe 13 dhidi ya Ihefu, na baada ya hapo mechi ya tarehe 20, tukichukua alama 6 kwenye mechi hizi tutakua pazuri sana” Ahmed Ally