Askofu Mkuu wa Kanisa la Methodist Tanzania, Joseph Bundala (55), amekutwa amejinyonga kwa kamba ndani ya ofisi yake iliyoko kwenye kanisani hilo, Mtaa wa Meriwa, jijini hapa.
Kiongozi huyo wa kiroho, ameacha waraka mrefu ukieleza sababu za kuchukua uamuzi huo kuwa ni madeni na mgogoro ulioko katika uendeshaji wa shule binafsi.
Bundala ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kanisa hilo kwa Afrika, mwili wake uligundulika juzi saa 1:00 usiku ukiwa unaning’inia ofisini kwake.
More On:ASKOFU MKUU AJINYONGA KISA MADENI/”AMEACHA WARAKA MZITO”
Akizungumzia tukio hilo jana, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Alchelaus Mutalemwa, alisema Jeshi la Polisi linachunguza tukio la askofu huyo, ambaye ni Mkazi wa Ihumwa jijini hapa kuchukua uamuzi huo.
“Tukio hilo liligundulika Mei 16, 2024 majira ya saa 1:00 usiku katika mtaa wa Meriwa, Dodoma, ndani ya ofisi yake iliyoko katika kanisa hilo. Uchunguzi katika eneo la tukio umekutwa ujumbe unaeleza sababu za kujinyonga ni madeni na mgogoro uliopo katika uendeshaji wa shule binafsi,” alisema.
Soma Zaidi:Aliyefariki Miaka Sita Iliyopita Aonekana Akichunga Ng’ombe
Alisema taarifa za awali hazijaeleza kiasi anachodai au kudaiwa kupitia ujumbe aliouacha.
More On:POLISI DODOMA WATOA TAARIFA KIFO CHA ASKOFU”NI KWELI AMEJINYONGA SABABU YA MADENI”
Akizungumza na Nipashe, Mwenyekiti wa Mtaa wa Sulungai, Grevas Lugunyale, alisema alipigiwa simu na mchungaji wa kanisa hilo kwa madai kuwa wamekuta Askofu amejinyonga.
“Nilipiga simu polisi kutokana na kukutwa amejinyonga. Katika ukaguzi tulikuta mezani kuna waraka ameuandika yeye mwenyewe. Kuna madai anadai na kuna madai naye anadaiwa. Polisi walipokuja pia walifanya uchunguzi wao tukahojiwa na kuchukua mwili kwenda kuuhifadhi,” alisema.
Alisema tukio kubwa na linaumiza kwa kuwa ni Askofu ambaye watu wengi wanamuamini na wanamjua lakini inaonekana hakuwa na watu wa kuwaambia yaliyomsibu ili apate ushauri ambao ungemsaidia.
Mwenyekiti wa Shina Namba 11, Jonathan Mpando, alisema anamfahamu Askofu Bundala amekuwa akisaidia kwenye kampeni kutokana na kuwa na kundi kubwa la waumini.
Jirani wa Askofu huyo, Kedmond Ngalya, alisema amejinyonga akiwa ofisi kwake na kuacha waraka ambao ulichukuliwa na polisi.
Naye jirani mwingine, Omar Hussein, alisema siku tatu zilizopita alikutana na Askofu huyo na walisalimiana na hakuonyesha dalili zozote za kukatisha maisha yake.
“Ila nimeshangaa taarifa ya kujinyonga kwake usiku ya jana (juzi) kusikia Askofu anayekemea dhambi ya kujinyonga na yeye amejitundika kwa kamba,” alisema.
Steve Magawa ambaye ni Jirani, alisema kifo hicho kimemsikitisha kwa kuwa kiongozi huyo wa dini alikuwa mwalimu wa matendo ya Mungu.
Katibu Mkuu wa Kanisa hilo, Allen Siso, alisema alipigiwa simu majira ya saa nne na mmoja ya watumishi na kwamba taarifa zaidi wataeleza baada ya kukaa kikao.