Operesheni na ukamataji uliofanywa na Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini ilifanikiwa kukamata dawa za kulevya za mashambani aina ya bangi na mirungi pamoja na dawa za viwandani aina ya heroin, cocaine, methamphetamine na dawa tiba zenye asili ya kulevya kama ilivyoainishwa
Katika mwaka 2023 kiasi cha tani 1,757.56 za dawa za kulevya aina ya bangi kilikamatwa kikihusisha watuhumiwa 8,803 kati yao wanaume 8,180 na wanawake 623. Aidha, katika kipindi hiki kumeibuka uingizaji na matumizi ya bangi mpya inayoitwa “skanka” ambayo inadhaniwa kuwa inazalishwa nchi za kusini mwa Afrika. Skanka ni mchanganyiko wa aina mbili za bangi, Cannabis sativa na Cannabis indica, ikiwa na kiasi kikubwa cha THC hivyo kuwa na athari kubwa zaidi kwa watumiaji.
View this post on Instagram
Mirungi ni dawa ya kulevya ya mashambani ambayo pia imeendelea kuwa tatizo kwa mwaka 2023. Mwaka 2023, jumla ya tani 202.74 za dawa hii zilikamatwa zikihusisha watuhumiwa 1,179 kati yao wanaume 996 na wanawake 183.
Soma: Afungwa Miaka 60 Jela:kosa Ukatili Wa Watoto
Kiasi cha bangi tani 1,757.56 kilichokamatwa mwaka 2023 ni zaidi ya mara tano ya kiasi kilichokamatwa kwa miaka tisa iliyopita kuanzia mwaka 2014 hadi 2022 ambacho kilikuwa tani 326.09. Aidha, kiasi cha mirungi tani 202.74 kilichokamatwa kwa mwaka mmoja wa 2023, kinazidi kiasi cha mirungi kilichokamatwa kwa miaka tisa iliyopita (kuanzia mwaka 2014 hadi 2022) ambacho kilikuwa tani 177.78. Mafanikio haya yametokana na juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ikiwemo uwezeshaji, utashi wa kisiasa na ushiriki wa wananchi katika kutoa taarifa.
I am truly thankful to the owner of this website who has shared this impressive article at at this place.