Ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa hatua ya robo fainali mkondo wa kwanza umemalizika jana kwa timu nane kumenyana kwenye viwaja tofauti.
Matokeo ya michezo ni Timu ya Kiduli FC iliibuka na ushindi wa magoli mawili kwa moja dhidi ya Elmerick iliyopata goli moja mchezo uliopigwa katika Uwaja wa Mwanambaya Mkuranga mkoani Pwani.
Aidha kwa upande wa Timu ya Mwalusembe ilipata ushindi wa magoli mawili kwa bila dhidi ya Mianzini mchezo huo ulipigwa katika Uwaja wa Mwanambaya Mkuranga mkoani Pwani.
Matokeo ya michezo mingine Nyika FC ambao walipata ushindi wa magoli matatu kwa bila dhidi ya Best Kids huku Thouth Academy ikitoka sare ya goli moja kwa moja dhidi ya Black Tiger michezo hii yote ilipigwa katika Uwanja wa Mwendapole Kibaha.
Hata hivyo michezo ya Mkondo wa pili hatua hii ya robo fainali itapigwa tena Disemba tisa na kumi katika viwanja vitatu vya Mwanakalenge, Mwanambaya na Mwendapole vilivyopangwa kufanyika kwa mashindano haya.
Imetolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano corefa.