Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishna Jenerali Thobias Andengenye imetakiwa kuachana na tabia ya kumaliza mashauri yanayohusu ukatili wa kijinsia nje ya mifumo ya kisheria na kusababisha usugu wa vitendo hiyo.
Kauli hiyo imetolewa kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku wa wanawake duniani yaliyofanyika kimkoa katika kata ya Makere wilayani Kasulu.
“Tafiti zinaonesha kuwa Asilimia Sitini (60%) ya matukio ya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia hufanywa katika ngazi ya familia huku kukiwa hakuna hatua zozote za kisheria zinazochukuliwa na kusababisha usugu wa tabia zinosababisha vitendo hivyo vyenye kuleta athari na maumivu ya muda mrefu miongoni mwa wanajamii” amesema Andengenye.
Aidha katika kufikia kasi ya mabadiliko ya kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa kundi hilo mkoani Kigoma, Mkuu huyo wa mkoa amewaelekeza wakurugenzi wa Halmashauri kuimarisha uratibu na usimamizi wa shughuli za kielimu, hamasa kuhusu uwekezaji na masuala ya usawa wa kijinsia kwa lengo la kuleta ustawi wa jamii.
Pia Andengenye amewaelekeza watendaji hao kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbli wa maendeleo katika kutekeleza mpango kazi wa Taifa wa kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto huku akiitaka jamii kutoendelea kufumbia macho vitendo hivyo kwani vina athari kubwa kwa watendewa.
Kwa lengo la kujiimarisha kiuchumi, Andengenye amekumbusha wanawake mkoani hapa kutumia fursa za maboresho makubwa ya miundombinu ya uchukuzi na Nishati ya Umeme, ili kujiletea maendeleo na Taifa kwa ujumla.
Kadhalika katika kuimarisha mfumo wa utawala bora, mkuu huyo wa Mkoa amewaasa wanawake mkoani hapa kushiriki chaguzi mbalimbali kwa lengo la kugombea nafasi za uongozi ili waweze kupata fursa ya kuonesha umahiri wao katika ngazi mbalimbali za kiutawala.
Additional source: Main fm