Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amewasili uwanja wa ndege wa Pemba na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mhe.Mattar Zahor Masoud na viongozi mbalimbali wa Serikali, Dini, Chama cha Mapinduzi na Vyombo vya Ulinzi na Usalama, punde baada ya kuwasili Rais Dk. Mwinyi ametembelea Dahalia la wavulana Skuli ya Sekondari Kengeja ambalo limeungua moto usiku wa tarehe: 31 Januari 2024, Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba.
Alipokuwa akiwatia moyo wanafunzi na walimu wa Skuli ya Kengeja, Rais Dk. Mwinyi ameahidi kujenga upya Skuli hiyo pamoja na dahalia iliyoungua moto.
Naye, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Lela Mohamed Mussa amewashukuru wadau mbalimbali waliojitolea michango akiwemo msamaria mwema aliyejitolea shilingi milioni 300, mfanyabiashara Rostam Aziz milioni 100, benki ya NMB wametoa magodoro 70 na mashuka 70, ZRA shilingi milioni 5, kampuni ya Vigor Group shilingi milioni 5, mfanyabiashara Hussein Muzzamil shilingi milioni 1, pamoja na KOICA wametoa sare za shule za wanafunzi 70.
Rais Dk.Mwinyi ameshukuru makampuni, wadau mbalimbali waliojitokeza na kuchangia misaada mbalimbali kwa ajili ya shule hiyo.