Dark
Light

Ofisi Ya Waziri Mkuu Yakanusha Taarifa ya Mikopo ya Mo Dewji

Ofisi ya Waziri Mkuu imekanusha taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii kupitia ukurasa wa Facebook uitwao "Mo Dewji Mikopo." Taarifa hiyo, iliyosambazwa na ukurasa huo, ilidai kuwa Mheshimiwa Waziri Mkuu alitoa kauli inayounga mkono taasisi hiyo.
April 6, 2024
by

Ofisi ya Waziri Mkuu imekanusha taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii kupitia ukurasa wa Facebook uitwao “Mo Dewji Mikopo.” Taarifa hiyo, iliyosambazwa na ukurasa huo, ilidai kuwa Mheshimiwa Waziri Mkuu alitoa kauli inayounga mkono taasisi hiyo.

Katika taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu, umma uliambiwa kuwa Mheshimiwa Waziri Mkuu hakutoa kauli yoyote kuhusu taasisi hiyo.

Read>> http://Waliobainika Kufanya Wizi Hatua Za Kisheria Zachukuliwa Dhidi Yao-Biteko

Bali wakati wa uzinduzi wa Programu ya IMBEJU mnamo Machi 12, 2023, jijini Dar es Salaam. Taarifa hiyo iliyosambazwa kwenye video ilikuwa na nia ya kuwahamasisha vijana kushiriki katika programu hiyo ya kuwawezesha kiuchumi.

Ofisi ya Waziri Mkuu ilisisitiza kuwa inathamini taasisi mbalimbali zinazotoa mikopo kwa makundi mbalimbali kupitia taratibu rasmi walizojiwekea. Wananchi wanaohitaji mikopo inashauriwa kutafuta taarifa kupitia Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, na ldara za Maendeleo ya Jamii zilizopo katika Halmashauri za wilaya zote nchini.

Read>> http://Man sentenced to death over murder

Taarifa hiyo pia ilionya dhidi ya matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii kwa kuchapisha habari za uongo na kuwahusisha viongozi wa Serikali. Ofisi ya Waziri Mkuu imechukua hatua kuzuia uenezaji wa taarifa za uongo na inasisitiza umuhimu wa upatikanaji wa taarifa sahihi na rasmi.

Kanusho hili la Ofisi ya Waziri Mkuu linaweka wazi kuwa Mheshimiwa Waziri Mkuu hakuwa na ushirika wowote na ukurasa wa Facebook wa “Mo Dewji Mikopo,” na wananchi wanahimizwa kupata taarifa za mikopo kupitia njia rasmi zilizopo

2 Comments

  1. What i don’t realize is actually how you’re now not actually much more well-appreciated than you may be right now. You are so intelligent. You understand therefore significantly on the subject of this topic, made me for my part consider it from so many varied angles. Its like men and women aren’t involved unless it is one thing to accomplish with Woman gaga! Your personal stuffs excellent. Always care for it up!

  2. I haven?¦t checked in here for a while since I thought it was getting boring, but the last few posts are good quality so I guess I?¦ll add you back to my daily bloglist. You deserve it my friend 🙂

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Don't Miss

BRICS Countries Now Control Over 20% of World’s Gold Reserves

According to a recent report from the World Gold Council,

Tanzania, Rwanda sign deal to boost dairy industry

Tanzania and Rwanda have signed a Memorandum of Understanding (MoU)