Mgogoro wa muziki wa Bongo Flava kati ya wasanii Billnass na Dulla Makabila umeendelea kupamba moto baada ya Dulla kumtuhumu Billnass kwa kudai kuwa ameiba wazo la wimbo wake.
Kulingana na Dulla, wimbo wa “Maboss” unaomshirikisha Billnass na Jux unachukua msukumo kutoka kwa kazi yake ya awali. Hata hivyo, Billnass amejibu vikali madai hayo, akikanusha na kudai kuwa wimbo wake hauna uhusiano wowote na wazo la Dulla.
Billnass amekanusha madai ya Dulla, akisisitiza kuwa idea ya wimbo huo haendani na ile ya Dulla na hivyo basi shutuma hizo hazina msingi. Zaidi ya hayo, Billnass ameamua kukata uhusiano wa kufanya kazi tena na Dulla, akimtaka kuachana naye na kumtafuta msanii mwingine kufanya naye kazi.
SomaZaidi;Usanga Katika Tuzo Za Albamu Bora 2023
Kando na hilo, Billnass ameenda mbali zaidi kwa kumtahadharisha Dulla, akimwambia kwamba hana utani linapokuja suala la kumchafulia jina lake. Hii inaashiria kuwa kuna uhasama unaokuwa kati yao ambao unaweza kuathiri sana uhusiano wao wa kibinafsi na hata kazi zao za baadaye.
Mgogoro huu umegawanya mashabiki wa muziki, baadhi wakiunga mkono Dulla na wengine wakimuunga mkono Billnass. Huku kila upande ukipigania haki yake, ni wazi kuwa mzozo huu unaweza kuwa na athari za kudumu katika tasnia ya muziki wa Bongo Flava. Tutashuhudia jinsi hali hii itakavyoendelea na jinsi itakavyowaathiri wasanii hawa na tasnia ya muziki kwa ujumla.