Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Urusi nchini, Mhe. Andrey Avetisyan kujadili masuala ya ushirikiano kati ya Tanzania na Urusi ikiwemo utalii.
Katika mazungumzo yao, Mhe. Makamba na Balozi Avetisyan wamejadili umuhimu wa kuendelea kuimarisha ushirikiano katika sekta ya utalii ikiwemo kuendelea kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini ili kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea nchini kutoka nchi hiyo.
Baadhi ya mambo yanayotazamiwa ni pamoja na kusaini Mkataba wa Ushirikiano katika Masuala ya Anga (BASA).
Mhe Waziri Makamba alitumia nafasi hiyo pia kutoa salamu za pole kwa Urusi kufuatia vifo vya watu zaidi ya 130 vilivyotokana na shumbilio la kigaidi lililotokea jijini Moscow hivi karibuni.