Mjadala wa bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025 ulioendelea Bungeni jijini Dodoma ulikuwa na mkondo wa kigeni baada ya Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini, Mhe. Mwita Waitara, kuelezea msimamo wake kuhusu suala la ushoga…..
Soma zaidi;British Soldiers In Kenya Have Unprotected Sex With Prostitutes For Initiation.
Katika mchango wake, Mhe. Waitara alihoji kwa nini Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Doroth Gwajima, hakuzungumzia suala hili katika hotuba yake wakati wa kuwasilisha makadirio ya mapato na matumizi. Mbunge Waitara amesema kuwa suala la ushoga ni changamoto ambayo nchi inakabiliana nayo na kwamba yeye mwenyewe yu tayari kushughulikia mtu yeyote anayehusika na vitendo vya ulawiti.
“Hatutaki Ushoga Tanzania, Wazungu waelewe kama ni misaada wanaleta wakome waache kabisa, Tusichekeane kama ni misaada Kataeni, Hii ni vita kama ilivyokuwa vita ya ukombozi wa bara la Afrika” alisema Mhe. Waitara katika mchango wake.
Tazama Zaidi:MWITA WAITARA “KAMA WAZUNGU WANATUPA MISAADA SABABU YA USHOGA BASI HATUITAKI”
Suala la ushoga limekuwa mada ya majadiliano na mabishano katika sehemu mbalimbali za ulimwengu kwa miaka mingi. Tanzania, kama nchi nyingine za Afrika, imeendelea kushikilia msimamo wake wa kuupinga ushoga kwa kuwa ni kitendo kinachokinzana na utamaduni na maadili ya jamii. Hata hivyo, wanaharakati wa haki za binadamu wameendelea kutetea haki za watu wenye unga wa jinsia, wakidai kuwa ni suala la haki za msingi za binadamu.
Mjadala huu uliendelea katika Bunge la Taifa, ikibainisha tofauti za maoni miongoni mwa wawakilishi wa wananchi kuhusu suala hili linaloendelea kugua gumzo ulimwenguni kote. Hii inaonesha kuwa masuala ya kijinsia na utambulisho wa kijinsia bado ni changamoto kubwa inayokabiliana na Tanzania na Afrika kwa jumla.
Hello! Someone in my Myspace group shared this website with us so I came to give it a look. I’m definitely enjoying the information. I’m book-marking and will be tweeting this to my followers! Great blog and brilliant design.