Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Paul Makonda amefanya kazi nzuri CCM akiwa Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa ya kukichemsha Chama na kufanya hata waliokuwa Wavivu kuamka ambapo amesema amempeleka Arusha kuwa Mkuu wa Mkoa na ana matumaini nae makubwa kuwa atafanya kazi nzuri kama aliyoifanya akiwa Mkuu wa Mkoa Dar es salaam.
Akiongea leo April 04,2024 Ikulu Dar es salaam wakati akiwaapisha Viongozi mbalimbali, Rais Samia amesema “Paul Makonda umefanya kazi nzuri CCM, umekichemsha Chama, ilikuwa Chama kidogo kina kila mmoja Mvivu kutoka hataki sinziasinzia lakini umeingia njiani umekichemsha Chama tumeamka vizuri sana lakini najua kwamba ulikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na kwenyewe ulifanya mazuri makubwa”
Read>> http://Makonda hints Possibility of Monthly Public Audience with Samia
Ameongeza kuwa “Tumekupeleka Arusha, unajua nini kipo Arusha na unajua matumaini yangu kwako Arusha, nenda kafanye kazi Arusha Mimi nina imani kubwa nawe na najua utafanya kile ambacho Mimi natamani ukafanye”
“Kubwa kwenye Arusha Utalii umekua vizuri sana, Wageni ni wengi malazi hakuna kwahiyo nenda kasimamie ukisaidiana na Uwekezaji kuhakikisha tunapata malazi mengi sana kwa ajili ya Wageni wetu, Arusha ni Mji Mkubwa sana ni Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki lakini Mataasisi mengi ya Kimataifa yapo Arusha kwahiyo nenda kasimamie vizuri Mkoa uwe na jina zuri” Amesema Rais Samia
Read>> https://mediawireexpress.co.tz/msafara-wa-makonda-wapata-ajali-masasi-mtwara/
Kumbukizi,Paul Makonda aliwahikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam,baada ya hapo alishika nyadhifa ya Katibu Itikadi,Uenezi na Mafunzo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kabla ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa Wa Arusha.
Hivyo hivyo Katika nafasi ya Katibu Itikadi,Uenezi na Mafunzo CCM alipata umaarufu zaidi kutokana na mtindo wake wa kutembea kwenye mikoa kutokana na kitu kinachopatikana mkoani hapo,pia alikuwa mtu wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua baadhi ya hizo na nyingine kuamrisha mamlaka husika kuchukua hatua stahiki pale panapoonekana kuna ukosefu wa haki.