Katika hatua muhimu ya kulinda watu wenye ualbino, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza viongozi wa mikoa na wilaya kuanzisha operesheni maalum za usalama katika maeneo yao.
Akizungumza Bungeni Majaliwa alisisitiza umuhimu wa serikali za mitaa katika kuhakikisha usalama wa watu hawa dhidi ya mashambulizi na vitisho.
Majaliwa alionyesha kuwa Mamlaka za Mikoa na Serikali za Mitaa zina jukumu la kusimamia, kulinda, na kutoa huduma kwa watu wenye ualbino. Alisema operesheni hizi zinapaswa kushirikisha vikosi vya usalama ili kutoa ulinzi kamili dhidi ya vitendo vya kikatili na ubaguzi ambao umekuwa ukiathiri jamii hii.
“Operesheni hizi lazima zihusishe vikosi vya usalama ili kuhakikisha ulinzi wa watu wenye ualbino dhidi ya mashambulizi na vitisho. Mamlaka za Mikoa na Serikali za Mitaa zina wajibu wa kusimamia, kulinda, na kutoa huduma kwa watu wenye ualbino,” alisema Majaliwa.
SomaZaidi;Polisi Afrika Mashariki Waungana Waadhimisha Mauaji Ya Kimbari
Waziri Mkuu alitoa wito kwa jamii kushiriki kikamilifu katika kuhakikisha usalama na haki za watu wenye ualbino, akieleza kuwa vitendo vya mauaji mara nyingi vinahusisha mitandao ya watu badala ya mtu mmoja mmoja. Alihimiza makundi na taasisi mbalimbali kushiriki kikamilifu katika vita dhidi ya ukatili huu.
Majaliwa pia aliomba viongozi wa dini kukemea mmomonyoko wa maadili unaosababisha ukatili huo. Aliwahimiza kutumia majukwaa yao ya ibada kuhubiri amani na ulinzi, akisisitiza kuwa kuumiza watu wasio na hatia, hasa wenye ualbino, ni kinyume na mafundisho ya dini.
“Nawasihi viongozi wetu wa dini tuungane kupambana na mauaji ya watu wasio na hatia