Dark
Light

Nchemba Awahakikishia Wafanyabiashara Usalama wa Kodi

Dkt. Nchemba, aliwaasa wafanyabiashara hao kuachana na mambo ya kuitisha migomo wanapotaka kuwasilisha hoja ama malalamiko yao badala yake watumie fursa na nia njema ya Serikali ya kuwasikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili kwa njia ya mazungumzo.
May 12, 2024
by
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), amewahakikishia wafanyabiashara nchini kuwa Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inatambua mchango mkubwa wa sekta binafsi hususani wafanyabiashara katika maendeleo ya nchi na kuahidi kuwa itaendelea kuzifanyiakazi changamoto zinazokwaza ustawi na mazingira ya ufanyaji biashara hususani kikodi.

Dkt. Nchemba alitoa ahadi hiyo jijini Dar es Salaam wakati Viongozi wa Wizara za kisekta wakiongozwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), walipokutana na Viongozi wa Kitaifa na wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo, jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine wamejadili masuala mbalimbali kwa jili ya kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara katika Soko hilo la Kimataifa.

Dkt. Nchemba, aliwaasa wafanyabiashara hao kuachana na mambo ya kuitisha migomo wanapotaka kuwasilisha hoja ama malalamiko yao badala yake watumie fursa na nia njema ya Serikali ya kuwasikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili kwa njia ya mazungumzo.

Aidha, aliwataka wafanyabiashara kuwa waaminifu na kulipakodi za Serikali kwa hiari ili fedha zinazopatikana zitumike kutekeleza miradi ya maendeleo.

Mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Tume ya Ushindani, Jijini Dar es Salaam, uliwashirikisha Viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Viwanda na biashara, Mhe. Dkt. AshatuKijaji (Mb), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. @kitilamkumbo (Mb), Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Daniel Sillo (Mb), Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. @albert_john_chalamila , Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah, Naibu Katibu Mkuu-Tamisemi (Miundombinu), Mhandisi Rogatus Mativila, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya na viongozi wengine waandamizi wa Serikali pamoja na wawakilishi wa Wafanyabiashara nchini pamoja na Soko Kuu la Kariakoo.11:47

2 Comments

  1. hi!,I love your writing so so much! percentage we be in contact extra approximately your post on AOL? I require a specialist in this house to resolve my problem. May be that’s you! Taking a look ahead to see you.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Don't Miss

Trump Urges France to Release Marine Le Pen

 U.S. President Donald Trump has publicly criticized the ongoing legal

 Tanzania’s Initiatives Shine at G20 Summit, Brazil

President Samia Suluhu Hassan of Tanzania is participating in the