Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob John Mkunda amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Usalama wa Jeshi la India, Luteni Jenerali Dokta Dinesh Singh Rana ofisini kwake, Upanga jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo yao, Jenerali Mkunda amesema kuwa ujio wake ni ishara ya kudumisha mahusiano kati ya Tanzania na India hasa katika nyanja za kidiplomasia ya kijeshi, mafunzo, kubadilishana uzoefu wa kijeshi na taarifa za kiusalama.
Mkuu wa Usalama wa Jeshi la India amefika ofisini kwa Jenerali Mkunda kumsalimia ikiwa ni sehemu ya ziara yake hapa nchini.
Soma:“Sehemu Nidhamu Imebaki Ni Katika Majeshi” Mwinyi
Sambamba na hilo Jenerali Mkunda amekutana na Mwambata Jeshi wa Jeshi la Malawi nchini Tanzania, Kanali Orion Msukwa alipofika ofisini kwake Upanga jijini Dar es Salaam kuaga baada ya muda wake wa kuliwakilisha Jeshi la Malawi hapa nchini kuisha.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano Makao Makuu – JWTZ
My spouse and I stumbled over here from a different website and
thought I should check things out. I like what I see so
now i’m following you. Look forward to looking at your web page repeatedly.