Jaji Abimbola Awogboro alitoa hukumu hiyo Jana Ijumaa Aprili 12.Tume ya Uhalifu wa Kiuchumi na Kifedha (EFCC), Alhamisi ya Aprili 4 Mwaka 2024, iliwasilisha mashtaka sita ya utakatishaji fedha na matumizi mabaya ya naira dhidi ya Mfanya biashara Huyo Wa Nguo Na Nyota wa Mitandao ya Kijamii mwenye Idadi Kubwa Ya Wafuasi.
More On: Mahakama ya Nigeria imemfunga miezi 6 jela cross-dresser Bobrisky kwa kurarua noti ya Naira
Siku ya Ijumaa, Aprili 5, EFCC ilimshtaki Bobrisky mahakamani kwa shtaka la makosa sita kuanzia Unyanyasaji wa Naira na utakatishaji fedha Huku Nyota Huyo Akikiri shtaka hilo la unyanyasaji wa Naira na kumfanya Jaji Awogbo aliyekuwa Mwndeshaji Wa Kesi Hiyo Kutoa Hukumu Hiyo.
Mahakama, hata hivyo, ilitupilia mbali mashtaka ya utakatishaji fedha lakini ikamtia hatiani kwa unyanyasaji wa Naira Punde tu baada ya kukiri kosa hilo.
Bobrisky aliyetambulika kwa jina la “Male” baada ya hakimu kumuuliza jinsia yake Mahakamani hapo, Aliiomba mahakama kuwa hafahamu sheria ya kutumia vibaya naira Na Laiti Angelifahamu Kosa Hilo Kabla Asingelitenda Nakujiweka Katika Matatizo Makubwa.
Aliongeza kuwa yeye ni mshawishi wa mitandao ya kijamii na wafuasi zaidi ya milioni tano Hivyo aliiomba Mahakama Kumpa Nafasi Ya Pili Kuelimisha Jamii Yake Juu Ya Kosa Hilo.
Jaji Awogboro alimwambia Bobrisky ya kwamba kutojua sheria haikuwa kisingizio cha kukiuka, Hivyo Utetezi Wake Hauna Mashiko Mbele Ya Mikono Ya sheria
Idris Okuneye Alisema Mbele Ya Mahakama (Nukuu),” namjua Bwana wangu. Bwana wangu, natamani ungenipa nafasi ya pili ya kutumia jukwaa langu kuwajulisha na kuwaelimisha wafuasi wangu kuhusu kumwaga pesa Chini.
“Ningefanya video kwenye ukurasa wangu na ningeelimisha watu kuhusu kunyunyizia pesa.
“Sitarudia, bwana wangu, najuta matendo yangu, bwana wangu.”
Baada ya Hukumu Hiyo Bobrisky Alipelekwa Kwenye Gari Ya Magereza Tayari Kwa Kupelekwa Gerezani Kuanza Kutumikia Hukumu Hio Huku Nje Ya mahakama Kukijawa Waandishi Wengi wa Habari Wakisubiri Hukumu Yake