Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe linamtafuta Masumbula Nemson, Mkazi wa Kitongoji C katika Kijiji cha Namkukwe, wilayani Songwe kwa tuhuma za kumuua mtoto wake wa miezi minne aitwaye Blasto Nemson, kwa kumpiga na fimbo kichwani upande wa kulia wakati akigombana na mama yake.
Ugomvi huo unaohusisha wivu wa mapenzi, unadaiwa kuibuka baada ya mtuhumiwa kumtuhumu mkewe kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mwingine.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Theopista Mallya, amesema tukio hilo limetokea Machi 8, 2024 majira ya saa 2:00 usiku na kwamba baada ya mtuhumiwa kufanya kitendo hicho alitorokea kusikojulikana.
“Upelelezi unaoambatana na msako mkali unaendelea kumtafuta mtuhumiwa na pindi akikamatwa atafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria” – amesema Kamanda Mallya.
Katika tukio hilo, pia mama wa marehemu alijeruhiwa kichwani na mikononi wakati akijikinga na kumkinga mtoto wakiwa wanashambuliwa kwa fimbo na mtuhumiwa.
Great site. Plenty of useful info here. I am sending it to some friends ans also sharing in delicious. And certainly, thanks for your sweat!
Having read this I thought it was very informative. I appreciate you taking the time and effort to put this article together. I once again find myself spending way to much time both reading and commenting. But so what, it was still worth it!