Dakika 90 za Mchezo wa Ligi kuu Soka Tanzania Bara kati ya Klabu ya Simba Dhidi ya Ihefu zimetamatika Kwa Sare Ya goli Moja Kwa moja Na Timu zote Kugawana Alama,
Ihefu Wakiwa Ndiyo Wenyeji Wa Mchezo Huko Liti Mkoani Singida walikuwa Wakwanza Kuandika Bao La Kuongoza Kupitia Mshambuliaji Wao Duke Abuya dakika ya 43, Huku Simba Wakichomoa Bao Hilo kwa Mkwaju Wa Penati Baada ya Mshambuliaji Wa Timu Hiyo Kibu Denis Prosper Kuchezewa Madhambi Ndani Ya eneo La 18 na Penati Hiyo kupigwa na Clatus Chota Chama Hivyo Mchezo Kufikia tamati ya sare.
More On:Simba SC kibaruani ikiwataja mashabiki
https://www.ippmedia.com/nipashe/michezo/soka/read/simba-sc-kibaruani-ikiwataja-mashabiki
Simba imebaki nafasi ya tatu Ikiwa na Alama 46, Huku Ihefu ikikwa hadi Nafasi ya nane ikifikisha Aalama 24 Katika msimamo wa Ligi, Huku Kinara akiendelea Kuwa Young Africans akiwa na alama 52 Akifatiwa na Timu ya Azam yenye alama 47.
Simba Imeendelea kupita kwenye zimwi la matokeo mabaya ya kufungwa pamoja na sare Katika Mashindano Tofauti Inayoshiriki Ikiwemo ligi ya Mabingwa Afrika,Ligi Kuu Tanzania Bara Pamoja na Kombe la Shirikisho la CRDB
Baada ya Matokeo hayo , mashabiki Wamekuwa na Mitazamo Mbalimbali Katika Mitandao Ya Kijami Juu ya Timu Hiyo Huku Wengi wakiikatia Tamaa katika Mbio Za Ubingwa wa Ligi Kuu , Ambalo ni Kombe Pekee Ambalo Timu Hiyo imebaki ikishiriki katika msimu huu,
Kwa Upande Mwingine Watani Wao Wajadi Wameendelea Kujinasibu Katika mitandao mbali mbali ya kijamii Baada Ya Sare hii, Wengi Wakisema Mechi ya mkondo Wa Pili Itakayo Wakutanisha Katika Uwanja Wa Benjamini Mkapa Itakuwa Nyepesi Mithili ya ile ya mzunguko Wa kwanza ambapo Yanga Aliibuka Na Ushindi Mnono wa Bao Tano kwa Moja, Ikumbukwe Wababe Hawa wa Kariakoo Watakutana Aprili 20 ya Mwaka 2024.
Mchezo Mwingine uliyochezwa mapema leo Muda Wa Saa nane Mchana ni kati ya Tabora United Dhidi Ya Jkt Tanzania, Ambapo Timu hizo Zimetoshana Nguvu kwa Kufungana Bao Moja Kwa Moja, Tabora Wakitangulia Dakika ya 72 Kwa Mkwaju Wa penati, Huku Jkt Wakichomoa Bao Dakika za Nyongeza.