Makatibu Wakuu wa sekta ya afya kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wamekutana kujadili pendekezo la kuanzisha vituo vya umahiri katika eneo hilo.
Mkutano huo ulifanyika jijini Arusha kwa lengo la kuandaa msimamo wa pamoja kabla ya Mkutano wa 7 wa Dharura wa Baraza la Kisekta la Mawaziri.
Pendekezo lililotolewa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linajumuisha kuanzishwa kwa Kituo cha Umahiri cha Sayansi ya Afya ya Kinywa chini ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), na Kituo cha Umahiri cha Upandikizaji Uloto na Sayansi ya Matibabu ya Magonjwa ya Damu chini ya Hospitali ya Benjamin Mkapa.
Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Grace Magembe, alieleza umuhimu wa vituo hivyo katika kuinua uwezo wa matibabu ya kibingwa, mafunzo ya kibobezi, na utafiti katika eneo la afya.
Mkutano huo ulisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kikanda katika kukabiliana na changamoto za afya na elimu, huku vituo hivyo vikionekana kama nguzo muhimu katika kufanikisha malengo hayo.
SomaZaidi;Mkutano wa Baraza La Mawaziri EAC Waanza Leo
Mwenyekiti wa kikao hicho, Katibu Mkuu wa Afya wa Jamhuri ya Sudan Kusini, Dkt. Ader Macar Aclek, alipongeza Tanzania kwa juhudi zake za kuongoza katika kuwasilisha pendekezo hilo na kusisitiza umuhimu wa ushirikiano katika kupambana na changamoto za kimataifa kama mabadiliko ya tabia nchi.
Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo uliongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Grace Magembe, na Naibu Katibu Mkuu wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. James Mdoe, pamoja na wataalamu wengine kutoka sekta za afya na elimu nchini.
Pendekezo hili linajiri wakati ambapo Jumuiya ya Afrika Mashariki inaendelea kujenga ushirikiano katika sekta mbalimbali kwa lengo la kuimarisha maendeleo ya kikanda. Hatua hii inaashiria mwanzo mpya katika kuboresha huduma za afya na kuwekeza katika rasilimali watu na utafiti katika eneo la Afrika Mashariki.
Hi , I do believe this is an excellent blog. I stumbled upon it on Yahoo , i will come back once again. Money and freedom is the best way to change, may you be rich and help other people.