Leo asubuhi katika mkutano wa waandishi wa habari, nyota wa Paris Saint-Germain, Kylian Mbappe, aliondoka kwa ghafla baada ya kuulizwa swali gumu kuhusu uwezekano wa kujiunga na Real Madrid. Swali hilo lilikuja baada ya PSG kutolewa katika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Borussia Dortmund, hivyo kusitisha matumaini yao ya kufika fainali.
Mbappe, ambaye amekuwa akifungia PSG kwa msimu huu, alikuwa akionekana kuwa mwenye wasiwasi tangu mwanzo wa mkutano huo, huku akipambana kujibu maswali ya waandishi wa habari. Hata hivyo, mambo yalichacha baada ya mwandishi mmoja kumuuliza ikiwa atashangilia Real Madrid dhidi ya Bayern Munich katika mechi ya leo. Mbappe alikosa jibu na badala yake akainuka na kuondoka huku akionekana kufadhaika.
Hili limeongeza uvumi kuhusu hatma ya Mbappe na uhusiano wake na PSG. Tangu msimu uliopita, kumekuwa na tetesi za mara kwa mara kuhusu uhamisho wake kwenda Real Madrid. Ingawa hakuna tangazo rasmi kutoka kwa pande zote mbili, tabia ya Mbappe leo inaashiria kuwa uhusiano wake na PSG unaweza kuwa umefikia mwisho.
Soma:Vita Ya Mfungaji Bora Ligi Kuu Yapamba Moto.
Usiku wa jana ulikuwa wa uchungu kwa PSG, ambao walishindwa kufunga licha ya kufanya majaribio 31 katika mchezo huo wa marudiano dhidi ya Dortmund. Bao pekee la Mats Hummels liliwapa Dortmund tiketi ya fainali kwa ushindi wa jumla wa bao 2-0. Hii ilikuwa pigo kubwa kwa PSG, ambao walikuwa wakilenga kufika fainali na hatimaye kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa.
Kwa sasa, macho yote yataelekezwa kwa hatua za Mbappe na mustakabali wake na PSG. Mashabiki wa soka wanasubiri kwa hamu kujua ikiwa ataendelea kubaki Paris au ikiwa ataanza sura mpya katika klabu nyingine. Kwa sasa, ni suala la kusubiri na kuona jinsi mambo yatakavyoendelea katika siku zijazo.
I appreciate, cause I found exactly what I was looking for. You’ve ended my four day long hunt! God Bless you man. Have a great day. Bye