Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa,ameeleza ni kwanini Rais Samia Suluhu Hassan atahutubia kwenye mkutano kati ya serikali ya Korea na wakuu wa nchi za Afrika, (African Summit) kuwa ni uwekezaji mkubwa uliofanywa kwenye miundombinu.
Akizungumzia na waandishi wa habari jijini Seoul, Korea, Mkurugenzi huyo alisema kwenye uwekezaji uliowekwa kwa Afrika Mashariki hakuna nchi inayoifikia Tanzania.
Soma Zaidi:Samia’s South Korea Trip To Yield Sh6.5 Trillion
Katika mkutano huo Rais Samia atatoa maoni katika jopo la Kuimarisha Usalama na Chakula na Madini.
“Uchaguzi kwamba Rais Samia atazungunza haijawa kwa bahati mbaya ni kwasababu watu wanajua kilichofanyika Tanzania hadi sasa.
Aidha, alisema Rais ameelekeza hadi Julai 14,2024 (Wiki mbili zijazo), treni ya SGR itaanza safari ya kutoka Dar hadi Morogoro, huku Morogoro hadi Dodoma ni Julai 25,2024
Mawaziri waliofuatana na Rais Samia ni Waziri wa Habari,Mawasiliano na Tekonolojia ya Habari,Nape Nnauye,Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais (Uwekezaji),Prof.Kitila Mkumbo, Waziri wa Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk.Ashatu Kijaji na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Fedha na Mipango Zanzibar, Dk.Saada Mkuya Salum.
I truly enjoy examining on this internet site, it holds fantastic content. “Those who complain most are most to be complained of.” by Matthew Henry.
Muchas gracias. ?Como puedo iniciar sesion?