Kesi inayomuhusu Waziri Mkuu wa zamani wa Burundi Jenerali Alain Guillaume Bunyoni inatarajiwa kusikilizwa leo baada ya kukata rufaa katika Mahakama ya rufaa.
Mahakama ya juu ya Burundi ilimuhukumu Waziri Mkuu wa zamani Alain-Guillaume Bunyoni kifungo cha maisha jela baada ya kumpata na hatia ya makosa kadhaa.
Read More:Burundi shuts border with Rwanda amid spat
Kwa mujibu wa duru za Mahakama ya juu ya Burundi, Bunyoni amepatikana na hatia ya Mashtaka kadhaa yaliyokuwa yakimkabili ikiwa ni pamoja na kujaribu kupindua serikali, kumiliki utajiri kinyume cha sheria na kuyumbisha uchumi.
Jenerali huyo wa zamani wa jeshi aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Burundi mnamo Julai 2020 na kufukuzwa kazi mnamo Septemba 2022.
Kuondolewa kwake kulikuja siku chache baada ya Rais Evariste Ndayishimiye kuonya juu ya kile alichokiita njama ya “mapinduzi” dhidi yake.
Dead pent content, thanks for selective information. “The bravest thing you can do when you are not brave is to profess courage and act accordingly.” by Corra Harris.