Bodi ya kusimamia ngumi za kulipwa nchini Uingereza imemfungia bondia Abdallah Pazi ‘Dullah Mbabe’ kuzichapa kwa muda nchini humo.
Read More: Msanii Harmonize Na Bondia Mwakinyo Wajipanga Kuzichapa
https://mediawireexpress.co.tz/msanii-harmonize-na-bondia-mwakinyo-wajipanga-kuzichapa/
Uamuzi wa bodi hiyo umekuja siku chache baada ya bondia huyo namba tatu nchini kwenye uzani wa super middle kupigwa kwa Knock Out (KO) ya raundi ya nne Machi 31, 2024.
Mbabe alichapwa na Callum Simpson bondia namba 36 dunia, kwenye uzani wa super middle na wanne nchini Uingereza mwenye nyota tatu.
Kwa mujibu wa mtandao wa ngumi za kulipwa wa dunia (Boxrec), bodi hiyo imemfungia mbabe kuzichapa Uingereza kwa muda.
Adhabu kama hiyo aliwahi kukutana nayo, Hassan Mwakinyo bondia namba moja nchini kwenye uzani wa super welter mara baada ya pambano lake la Septemba 3, 2022, alipochapwa kwa Technical Knock Out (TKO) ya raundi ya nne la Liam Smith nchini humo.
Read More: Mwakinyo yuko tayari kupambana na mpinzani wake
Hata hivyo sababu za zimetofautiana kutokana na maelezo ya bodi ya ngumi nchini Uingereza uchunguzi umebaini kwamba Mwakinyo Alidanganya “cheat” kiatu alichopewa hakikuwa na madhara yoyote, hata hivyo alipatiwa kabla ya siku ya pambano hivyo alikijaribu na kujiridhisha kipo sawa.
Hivyo mwakinyo kafungiwa kucheza michezo ya ngumi Uingereza kwa mujibu wa kanuni zinazozingatia ‘Fair play”
Sababu ya pili iliyogundulika ni mazingira ya kuuza mechi! Hili nalo limechangia Mwakinyo afungiwe
Taarifa za kitabibu kutoka maabara ya uwanja wa ndege zilizobaini begi la Mwakinyo halikuwa na vitu vya kawaida kimchezo ambavyo vimetafsiliwa ni ushirikina katika mchezo.
Hata hivyo, Rais wa Kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania (TPBRC), Chaurembo Palasa amefafanua chanzo cha adhabu hizo kuwa zinatolewa ili kulinda afya ya bondia baada ya kipigo na ndicho kimetokea kwa Dullah Mbabe.
I believe this internet site has some really excellent info for everyone :D. “Nothing great was ever achieved without enthusiasm.” by Ralph Waldo Emerson.