Mbunge wa Kisesa (CCM), Luhaga Mpina, alitoa taarifa muhimu kwa vyombo vya habari kuhusu utaratibu uliotumika kuagiza sukari nchini ambapo kampuni iliyosajiliwa kuuza simu ilichukua zabuni ya kuagiza bidhaa hiyo, hayo amesema alipokutana na wanahabari jijini Dodoma leo, Ijumaa, Juni 14, 2024,
“Bodi ya sukari ilisajili makampuni kuingiza sukari ambayo hayakuwa na sifa kisheria na makampuni hayo hayakuwa na rekodi yoyote ya kujihusisha na biashara ya sukari na pia uwezo wao wa kifedha ni wa kutiliwa mashaka jambo ambalo ni kinyume cha sheria ya sukari, baadhi ya makampuni machache yaliyopewa vibali vya kuingiza sukari nchini ambayo hayana viwanda vya kuzalisha sukari nchini ni pamoja na kampuni ya ‘Itel East Africa Limited’ ambayo Bodi ya sukari ilimuandikia barua yenye Kumb. Ref. No. SBT/DGO/09/VOL.II/2-10 ya tarehe 2 Januari 2024 iliyosainiwa na Lusomyo Buzingo kwa niaba ya Mkurugenzi mkuu wa Bodi wa sukari ikiitarifu kampuni hiyo kuwa serikali imeidhinisha kuingiza tani 50,000 za sukari” -Mpina
“Lakini tarehe 9 Januari 2024 na tarehe 30 Januari 2024 kampuni ya ‘Itel’ ilipewa vibali vya kuingiza tani 60,000 za sukari zaidi ya kiwango kilichoidhinishwa kwenye barua rejea kibali SR Na. 8652445335 na 944600548 pia vibali alivyopewa Itel ni zaidi ya viwanda vyote vitano ambavyo jumla vimepewa tani 50,000 tu kwa maana ya tani 10,000 kila kiwanda, baada ya kufanya upekuzi wa BRELA tarehe 10 Juni 2024 ilibainika kuwa kampuni ya Itel East Africa Limited imesajiliwa tarehe 15 Februari 2013 yenye ofisi zake Ilala, Dar es Salaam kwa ajili ya biashara za kuuza rejareja simu, komputa, TEHAMA na vifaa vingine vya mawasiliano na sio biashara ya sukari, Wzara ya Kilimo na Bodi ya sukari wameipa kampuni ya Itel kuagiza sukari wakati ni kampuni ya kuuza simu na kampuni hiyo haina uwezo, ujuzi na weledi wa masuala ya sukari na hivyo inaweza kupelekea kuingiza sukari isiyo na ubora, kufanya udanganyifu, kukwepa kodi na kuliingiza Taifa katika migogoro ya kibiashara kimataifa” -Mpina
“Kampuni ya Itel Easr Africa Limited 49% ya hisa zinamilikiwa na raia wa India, viwanda vya ndani vinavyolipa kodi, soko la wakulima wa miwa na kutoa ajira kwa Watanzania wengi vimeachwa na kipaumbele kupewa makampuni binafsi, kampuni ya Itel East Africa Limited ina hisa za kawaida 1000 zenye thamani ya Tsh. 50,000,000, kampuni hii ina mtaji mdogo na sijaona ushahidi wa kuongeza mtaji na hivyo haiwezekani kupewa kazi ya zaidi ya shilingi bilioni 160 kwa mara moja nimefuatilia ‘Financial Statements’ za be mwaka 2020, 2021, 2022, 2023 inaonyesha kampuni inafanya biashara ndogo na haina uwezo mkubwa kifedha, kitendo cha kupewa vibali vya kuagiza sukari kwa mara moja zenye thamani ya shilingi bilioni 160 kupitia kampuni hii inaweza ikawa ni utakatishaji wa fedha haramu, kufanya udanganyifu na kukwepa kodi” -Mpina
“Kampuni ya Itel East Africa Limited ilihuisha taarifa zake tarehe 19 Februari 2024 siku chache baada ya kupewa barua na vibali vya kuingiza sukari nje ya nchi kati ya tarehe 9 na 30 Januari 2024, pengine ilikuwa kutafuta sifa za ziada, barua ya Bodi ya sukari yenye Kumb. Ref. No. SBT/DGO/09/VOL.II/2-10 ya tarehe 2 Januari 2024 iliyoijulisha kampuni ya Itel kuruhusiwa kuagiza sukari nje ya nchi haionyeshi kama kampuni hiyo iliwahi kuomba kibali cha kuagiza sukari kutoka nje ya nchi, haya ni matumizi mabaya ya madaraka na inaweza kuwa kula njama kuiibia serikali (organized crime), hata hivyo zipo taarifa kuwa kampuni ya Itel East Africa Lts inatumiwa na kampuni ya Mohammes Enterprises (T) Ltd kwa mgongo wa nyuma kuagiza sukari nje ya nchi kwa niaba yake, taarifa za mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) zinaonyesha kuwa mzigo wa sukari wa kampuni ya Itel ukifika Bandarini unatolewa na kampuni ya METL rejea, pia ziko taarifa za uhakika kuwa baada ya mzigo kutolewa Bandarini unapelekwa kwenye ICD ya Mohamed Enterprises na kutoka ICD sukari inapelekwa kwenye godown za Mohamed Enterprises na baadaye kuuzwa rejareja na jumla, mahusiano ya kibishara baina ya kampuni ya Mohammed Enterprises (T) Ltd na Itel East Africa Ltd hayako wazi na yanaweza ikawa ni mkakati wa kutakatisha fedha haramu na kukwepa kodi za serikali” -Mpina