Waziri wa Kilimo Hussein Bashe ametolea ufafanuzi kauli yake aliyoitoa jana kuhusu sukari kupatikana mwezi wa Ramadhani wakati akijibu swali kwenye mkutano na wahariri wa vyombo vya habari uliofanyika Ikulu Dar es Salaam.
Hivyo Waziri Bashe amesema kauli yake haikuhusianisha udini bali alitumia kama kiashiria cha muda wa upatikanaji wa bidhaa hiyo.
“Ningependa kutoa ufafanuzi wa kauli yangu iliyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari wakati wa maswali na majibu kwenye mkutano na wahariri uliofanyika Ikulu, Dar es Salaam tarehe 22.02.2024”. Amesema
“Kama Waziri wa Kilimo, nilitoa maelezo juu ya hali ya upungufu wa Sukari nchini, na muda wa usambazaji tunaotarajia wa shehena inayofuata ya sukari”.amesema
“Nilisisitiza kuwa kutokana na usambazaji huu na hatua tulizochukua, tutarajie hadi kufikia mwezi mtukufu wa Ramadhan hali itakua nzuri”.amesema
“Rejeo hili lilikusudiwa kuwa kiashiria cha MUDA kwa madhumuni ya kimipango na sio kuashiria kipaumbele chochote cha KIDINI.”amesema
“Mara kadhaa nimesisitiza kwa kutaja vipindi vyote viwili Kwaresma na Ramadhani vina tukabili hapo mbeleni na kuwa tunajitahidi kama Serikali na azma yetu ya kutaka kutatua hii changamoto kabla ya hivi vipindi kufika na ndio maana tulianza kutoa vibali tangu mwezi wa 12, 2023.” Waziri Bashe