Mpira wa miguu wa Cameroon ulizidi kuzama katika mgogoro siku ya Jumanne wakati mkutano kati ya rais wa chama cha mpira wa miguu Samuel Eto’o na kocha mpya wa Kibelgiji Marc Brys ulipogeuka kuwa mvutano wa hasira.
Ilikuwa mara ya kwanza kwa Eto’o kukutana na Brys, ambaye aliteuliwa na wizara ya michezo ya nchi hiyo mapema April bila ushirikiano wowote kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu la Cameroon, kusababisha mzozo kati ya hao wawili.
Soma Zaidi:Paul Pogba has been banned from football for four years
Brys alikuwa amealikwa kwa “kikao cha kufanya kazi” na Eto’o wakati Cameroon wanajiandaa kwa mechi za kufuzu Kombe la Dunia mwezi ujao, lakini baadhi ya wasaidizi wa kocha huyo waliochaguliwa na wizara ya michezo, walikatazwa kuingia jengo la shirikisho la FECAFOOT huko Yaounde.
Tazama Video:Eto’o Amvaa Kwa Maaneno KochaMpya Wa Cmeroon
Video zilizosambazwa kwenye mitandao kadhaa ya kijamii, zilizopigwa na waandishi wa habari, zinaonyesha Eto’o akimkaribisha Brys lakini ghafla Eto’o akaanza kumtupia maneno kocha Huyo akionekana kuwa na hasira.
Kwanza Eto’o alimfukuza kwa hasira afisa wa wizara ambaye alitaka kuhudhuria mkutano, na punde tu wakavaana kwa kubadilishana maneno na kocha Brys, ambaye aliondoka mara moja.
Samuel Eto’o ni rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Cameroon Alilaani uteuzi wa kocha ahuyo kwa hoja ya uamuzi wa upande mmoja na waziri wa michezo Narcisse Mouelle Kombito.
Kawaida, shirikisho la mpira wa miguu lingeteua na kulipa makocha wake lakini katika nchi kadhaa za Kiafrika hii inafanywa na serikali, hasa wakati mashirikisho yanakabiliwa na ukata.
Mchezaji wa zamani wa Afrika wa Mwaka Eto’o, ambaye alikuwa na kazi nzuri akiichezea Ulaya, amejaribu kudai uhuru fulani lakini pia amelazimika kuchukua tahadhari katika nchi ambapo masuala yanayohusu timu ya taifa ni ya kipaumbele kwa serikali.
Timu ya taifa ya Cameroon Walipata ushindi dhidi ya Mauritius nyumbani na sare ugenini na Libya katika mechi zao mbili za kwanza za kufuzu Kundi D mwezi Novemba chini ya Rigobert Song, ambaye mkataba wake haukuongezwa baada ya Cameroon kutolewa katika raundi ya 16 kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwezi Januari.