Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, John Mongella amewataka Wanachama wa CCM wamuamini huku akiwaahidi kuwa atasimamia kuhakikisha utendaji ndani ya Chama hicho na kuipongeza safu ya uongozi iliyoteuliwa hivi karibuni na sekretarieti.
Mongella ameyasema hayo leo Aprili 5, 2024 Jijini Dar es salaam wakati wa mapokezi ya Sekretarieti ya CCM huku akibainisha kuwa kumekuwa na maeneo Wana CCM wanatishwa kitoto ambapo amewataka wasikubali kutishwa na yoyote.
“Mimi kwa nafasi yangu kama Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara sio Mtu wa majukwaa sana, niwaahidi nitasimamia kuhakikisha utendaji ndani ya Chama chetu unaakisi ukubwa wa Chama, kama Mtu ana akili timamu baada ya kumsikia Jokate, Ally Hapi, Makalla maana yake muziki umeanza na Mimi nataka kusema kama kuna Mtu alikuwa hamuelewi vizuri Mh. Rais Dkt. Samia hii safu ni ujumbe tosha”
Read>> http://New CCM Secretary General sets the tone
“Kazi yetu ni kujipanga na Wana CCM tuwe na kujiamini, kuna maeneo Wana CCM wanatishwa kitotototo, tusikubali kutishwa na yeyote, Mimi nakumbuka tulipiga marufuku Watu kutishwa hapa Mjini ilikuwa marufuku Watu kutishwa Mtu akitaka aje kistaarabu, Vijana lazima tusimame kukilinda Chama”
“Na mmepata Katibu Mkuu imara, Mwenyekiti imara, Viongozi imara, UVCCM mna jukumu la kulinda Viongozi wa Chama na mali za Chama, wote tuna Dini zetu na Madhehebu yetu lakini CCM sio Dhehebu ina kazi ya kutafuta Dola, kwahiyo katika kushika Dola hakuna kubembelezana”
Read>> http://Untold story over CCM-CHADEMA reconciliation talks
“Hakuna Shangazi wala Mjomba, tukimaliza kushika Dola Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu tutakuja tutakaa mezani tutakunywa kahawa, na jambo hili wala halina mzaha lakini kama wenzangu walivyosema Mh. Rais ni Muumini wa maridhiano na mapatano na demokrasia ya kweli”
“Tungeomba wote uwe mwelekeo wetu mpaka Vyama rafiki, lakini pale Mtu akikata kwenda vinginevyo sisi huku hasa kwenye Sekretarieti hii utaalamu upo wa kutosha wa hayo mengine lakini tutakuwa Wavumilivu kwasababu Mwenyekiti wa Chama chetu anaamini katika hilo lakini ushindi wa CCM ni lazima wala halina mjadala”
Some really interesting info , well written and broadly user genial.
Can you be more specific about the content of your article? After reading it, I still have some doubts. Hope you can help me.
Your point of view caught my eye and was very interesting. Thanks. I have a question for you.