Dark
Light

DK.Mwinyi Asisitiza Kudumisha Muungano

Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa umoja wa Watanzania unazidi kuimarika , ushirikiano katika shughuli mbalimbali unaongezeka na amani inaendelea kudumu nchini.
April 14, 2024
by

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema ni wajibu kuulinda Muungano, kuuendeleza, kuudumisha na kuimarisha zaidi ili kuzidi kunufaika kwa dhamira ile ile ya Waasisi wa Taifa letu.

Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa umoja wa Watanzania unazidi kuimarika , ushirikiano katika shughuli mbalimbali unaongezeka na amani inaendelea kudumu nchini.

Read More: “Sehemu Nidhamu Imebaki Ni Katika Majeshi” Mwinyi

https://mediawireexpress.co.tz/sehemu-nidhamu-imebaki-ni-katika-majeshi-mwinyi/

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipofungua Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Maonesho ya Taasisi mbalimbali viwanja vya Nyamanzi , Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe: 14 Aprili 2024.

Aidha Rais Dk.Mwinyi amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zimeendelea kuchukua hatua madhubuti za kuzitafutia ufumbuzi changamoto zote zinazojitokeza katika utekelezaji wa masuala ya Muungano.

Halikadhalika Rais Dk.Mwinyi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuweka vipaumbele masuala ya kuimarisha Muungano.

Rais Dk.Mwinyi amesema Tanzania imefikia mafanikio makubwa kipindi cha Miaka 60 katika nyanja zote za maendeleo ya kisiasa, kiuchumi na huduma za jamii.

Read More: Mwinyi Woos Investors In Oil, Gas

https://mediawireexpress.co.tz/mwinyi-woos-investors-in-oil-gas/

Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amewahimiza wananchi kuendelea kushiriki shamrashamra za sherehe za miaka 60 ya Muungano katika Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar ikiwa ni pamoja na siku ya kilele tarehe 26 Aprili, 2024 katika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam ambapo Mgeni Rasmi atakuwa Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Rais Dk.Mwinyi amesema kipindi cha miaka mitatu, 2021 hadi mwaka 2024 hoja 15 zimepatiwa ufumbuzi kati ya hoja 18 zilizokuwepo.

Vilevile Rais Dk.Mwinyi amesema Tanzania imeendelea kubaki katika historia na mfano bora wa kudumisha Muungano barani Afrika na Duniani kote.

3 Comments

  1. Howdy! Someone in my Facebook group shared this website with us so I came to give it a look. I’m definitely loving the information. I’m book-marking and will be tweeting this to my followers! Wonderful blog and outstanding design and style.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Don't Miss

Tanga Port Supports Malawi with Urgent Fuel Shipment

Malawi has turned to Tanzania’s Tanga Port to secure an

Hadzabe and Tatoga Communities Face Existential Threats

Tanzania, a country known for its rich diversity with over