Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inatangaza kwamba tarehe 8 Aprili 2024 kutatokea tukio la kupatwa kwa Jua kikamilifu katika sehemu ya Bara la Amerika ya Kaskazini. Kupatwa kwa Jua ni tukio ambapo kivuli cha mwezi huangukia juu ya uso wa Dunia, na katika maeneo yaliyo ndani ya kivuli hicho, Jua huonekana likifunikwa na Mwezi kwa kipindi cha saa chache.
Kuna aina mbili za kupatwa kwa Jua: kupatwa kwa Jua kikamilifu na kupatwa kwa Jua Kipete. Kupatwa kwa Jua kikamilifu hutokea wakati mwezi huzuia kabisa mwanga wa Jua kufika katika Dunia, wakati kupatwa kwa Jua Kipete hutokea wakati mwezi huzuia sehemu tu ya mwanga wa Jua, hivyo kutengeneza umbo la pete la mwanga wa Jua angani.
Read>> Majaliwa aweka jiwe la msingi jengo la TMA
http://Majaliwa aweka jiwe la msingi jengo la TMA
Tukio la kupatwa kwa Jua Kikamilifu litatokea Jumatatu, tarehe 8 Aprili 2024. Njia ya kupatwa kwa Jua itaanza katika maeneo ya kusini mwa Bahari ya Pasifiki, ambapo Mexico itakuwa nchi ya kwanza kufikiwa na kupatwa kwa Jua Kikamilifu majira ya saa 5:07 asubuhi kwa saa za Amerika. Baadaye, njia hiyo itaendelea kupitia Texas, Marekani majira ya saa 7:40 mchana, na kuingia Kusini mwa Ontario, Kanada. Hatimaye, kupatwa kwa Jua Kikamilifu kutatoka Bara la Amerika ya Kaskazini kupitia pwani ya Bahari ya Atlantiki huko Newfoundland, Kanada, saa 11:16 jioni.
Ni muhimu kutambua kwamba Tanzania haitashuhudia tukio hili la kupatwa kwa Jua Kikamilifu. Kwa kuwa nchi yetu iko mbali na njia ya kupatwa kwa Jua, hatutakuwa na uwezo wa kuona tukio hilo. Athari za moja kwa moja za tukio hili katika masuala ya kijamii na kiuchumi hazitarajiwi kuonekana hapa nchini.
Kwa habari zaidi kuhusu kupatwa kwa Jua Kikamilifu, tunakuhimiza kutembelea tovuti yetu rasmi mamlaka ya.hali ya hewa Tanzania TMA.
Read>> Mchengerwa Atoa Milioni 40 Wusaidia Wahanga Wa Mafuriko Rufiji
http://Mchengerwa Atoa Milioni 40 Wusaidia Wahanga Wa Mafuriko Rufiji
Wow that was unusual. I just wrote an really long comment but after I clicked submit my comment didn’t show up. Grrrr… well I’m not writing all that over again. Anyhow, just wanted to say superb blog!
It’s actually a great and helpful piece of info. I am glad that you shared this helpful info with us. Please keep us informed like this. Thanks for sharing.
Can you be more specific about the content of your article? After reading it, I still have some doubts. Hope you can help me.