Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Filipe Nyusi, anatarajia kuwasili nchini Kesho Julai 01, 2024 kwa ajili ya kuanza ziara yake ya Kikazi ya takribani Siku 4 nchini, kufuatia Mwaliko rasmi wa Rais wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Januari Makamba amebainisha hayo leo Juni 30, 2024 Jijini Dar es Salaam wakati akielezea Ujio wa Rais Filipe Nyusi.
Soma: Makamba Awasili China kwa Ziara ya Kikazi
Waziri Makamba amesema Rais Nyusi anakuja nchini kwa Sababu kuu mbili ambazo ni Ziara ya Kitaifa ‘State Visit’ pamoja na Kufungua Rasmi Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa Maarufu kama ‘Saba saba’.
“Kama nilivyosema nchi ya Msumbiji ni Taifa Rafiki kwa Tanzania Kihistoria kwa hiyo ziara hii ni muhimu kwake kwa Sababu anakwenda kuhitimisha Muhula wake wa Pili Mwezi Oktoba mwaka huu akiwa Kiongozi wa Juu wa Msumbiji, kwa hiyo pia anatumia Fursa hiyo kuja Kuwaaga Watanzania” amesema Waziri Makamba.
Excellent read, I just passed this onto a friend who was doing a little research on that. And he just bought me lunch as I found it for him smile So let me rephrase that: Thank you for lunch! “Dreams are real while they last. Can we say more of life” by Henry Havelock Ellis.